Eric Aniva akiwa nje ya mahakama ya Nsanje mwezi Agosti 2016
Uamuzi wa kesi ya mwanamme mmoja nchini Malawi unatarajiwa kutolewa wiki
hii, baada ya kuiambia BBC kuwa alifanya mapenzi na wasichana kama
sehemu ya mila.
Eric Aniva alikamatwa mwezi Julai kufuatia amri ya rais, baada ya kukiri
kuwa alifanya mapenzi yasiyo na kinga na wasichana walio na umri wa
hadi miaka 12, na kuwa kimya juu ya hali yake ya kuugua ugonjwa wa
ukimwi.
Aniva anasema kuwa alipewa vibarua na familia za wasichana hao kushiriki
mapenzi nao, kwa tamaduni ambayo jamii inaamini kuwa huwezesha
wasichana kuingia utu uzima.
"Tunaamini kuwa ikiwa mjane au mwanamme aliyefiwa hawezi kusafishwa kwa
njia ya mapenzi, huenda kisa kibaya kikafuatia kama kifo kwa majane au
mwanamme aliyefiwa au kwa ukoo mzima," alisema mhudumu mmja wa jamii.
Wakati rais wa Malawi Peter Mutharia aliamrisha mwanamme huyo akamatwe,
alitaka Aniva ashtakiwe kwa kuwabaka wasichana wadodgo, lakini hata
hivyo hakuna msichana aliyejitokeza kutoa ushahidi dhidi yake.
Kwa hivyo sasa Aniva ameshtakiwa kwa kushiriki utamaduni wenye kuumiza,
chini ya kipengee cha chato cha sheria ya usawa wa kijinsia nchini
Malawi ambapo alifanya mapenzi na wajane.
Katika kesi hii wanawake wawili wamejitokeza ili kutoa ushahidi dhdi ya
Aniva, licha ya mmoja kusema kuwa alifanya mapenzi naye kabla ya mila
hiyo kupigwa marufuku huku mwingine naye akisema kuwa alifanikiwa
kukimbia kabla ya kitendo cha ngono kufanyika.
Hadi miaka michache iliyopita, mila hii ilikuwa maarufu katika wilaya
yote kwa mjane kufanya mapenzi na mwanamme mara tatu kwa siku kwa usiku
tatu au nne.Image copyrightAFPImage capti
Mwanamme huyo anaweza kuwa ndugu wa mmewe, lakini wakati mwingine mtu
kutoka nje hutafutwa kama Aniva kuweza kushiriki kitendo hicho.
Ikiwa aliyefiwa ni mwanamme, mwanamke hutafutwa kuweza kufanya mapenzi naye.
Kinachowatisha watu nchini Malawi kuhusu Aniva, ambaye alidai kufanya
mapenzi na wanawake 104 pamoja na wasicha, wakati wa mahojiano na BBC ni
kuwa hukuachana na tabia hiyo licha ya kugundua kuwa alikuwa na virusi
vya HIV
"HIV inaua. Itakuwaje mtu mwenye virusi kufanya kile alichokifanya?
Nafikiri yeye ni shetani. Ningekuwa hakimu ningempa hukumu ya kifo na
kifungo cha maisha," alisema mhubiri Paul Mzimu.
Chanzo-BBC
No comments:
Post a Comment