KOMBE LA DUNIA 2018: RONALDO AIONGOZA VYEMA PORTUGAL, DEPAY AIPA USHINDI NETHERLANDS, BELGIUM WASHUSHA 8! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, November 14, 2016

KOMBE LA DUNIA 2018: RONALDO AIONGOZA VYEMA PORTUGAL, DEPAY AIPA USHINDI NETHERLANDS, BELGIUM WASHUSHA 8!




ULAYA – KOMBE LA DUNIA 2018 – Makundi:
Matokeo:
Jumapili Novemba 13
Bulgaria 1 Belarus 0
Luxembourg 1 Netherlands 3
Hungary 4 Andorra 0
Switzerland 2 Faroe Islands 0
Portugal 4 Latvia 1
Cyprus 3 Gibraltar 1
Belgium 8 Estonia 1
Greece 1 Bosnia And Herzegovina 1
++++++++++++++++++++++++
MABINGWA wa Ulaya Portugal, Netherlands, Belgium na Uswisi Jana zilishinda Mechi zao za Makundi katika mbio zao za kufanikiwa kucheza Fainali za Kombve la Dunia huko Russia Mwaka 2018.

Portugal, wakicheza kwao, waliifumua Latvia 4-1 katika Mechi ya B ambao Cristiano Ronaldo alifunga Bao 2, moja likiwa Penati, na pia kukosa Penati moja.
Bao nyingine za Portugal zilifungwa na Carvalho na Bruno Alves.

Kwenye Mechi nyingine ya Kundi B, Usisi iliipiga Faroe Islands 3-0 na kujikita kileleni wakiwa na Pointi 12 na kufuata Portugal wenye 9.

Kwenye Kundi A, Netherlands wamekiweka Nafasi ya Pili nyuma ya France baada ya kuifunga Luxembourg 3-1 huko Memphis Depay wa Man United akipiga Bao 2 na la 3 kufungwa na Arfen Robben
++++++++++++++++++++++++
JE WAJUA?
-Ulaya itakuwa na Nafasi 13 kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia
-Washindi wa Makundi 9 watatinga moja kwa moja Fainali za Kombe la Dunia
-Washindi wa Pili 8 wa Makundi watacheza Mechi za Mchujo kupata Washindi Wanne kwenda Fainali za Kombe la Dunia
++++++++++++++++++++++++

Kwenye Kundi H, Belgium wamezidi kupaa kileleni baada ya kuicharaza Estonia 8-1 kwa Bao 2 kila mmoja za Dries Mertens na Romelu Lukaku, na moja moja za Thomas Meunier, Eden Hazard na Yannick Carrasco huku Ragnar Klavan akijifunga mwenyewe na kuipa Bao Estonia.
ULAYA – KOMBE LA DUNIA 2018 – Makundi:
Matokeo
Ijumaa Novemba 11
France 2 Sweden 1
Czech Republic 2 Norway 1
Northern Ireland 4 Azerbaijan 0
San Marino 0 Germany 8
Armenia 3 Montenegro 2
Denmark 4 Kazakhstan 1
Romania 0 Poland 3
England 3 Scotland 0
Malta 0 Slovenia 1
Slovakia 4 Lithuania 0
Jumamosi Novemba 12
Austria 0 Ireland 1
Georgia 1 Moldova 1
Wales 1 Serbia 1
Albania 0 Israel 2
Liechtenstein 0 Italy 4
Spain 4 Macedonia 0
Croatia 2 Iceland 0
Turkey 2 Kosovo 0
Ukraine 1 Finland 0

No comments:

Post a Comment