MABINGWA wa Soka Tanzania Bara, Yanga, wamewatambulisha rasmi Hans van de Pluijm na George Lwandamina kama Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha Mkuu katika Hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Yanga, Mitaa ya Jangwani na Twiga Jijini Dar es Salaam.
Mholanzi Hans van de Pluijm, ambae alikuwa Kocha Mkuu, sasa ‘anapanda ghorofani’ na kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Raia wa Zambia George Lwandamina anakuwa Kocha Mkuu.
Lwandamina, ambae alikuwa Kocha wa ZESCO huko kwao Zambia na sasa anamrithi Pluijm, amesema hatabadili Benchi lake la Ufundi na atashirikiana vyema na Pluijm.
Kauli hiyo inamaanisha Wasaidizi wa Lwandamina watabaki kuwa Watu walewale waliokuwa chini ya Pluijm ambao ni Juma Mwambusi, Kocha Msaidizi, Juma Pondamali, Kocha wa Makipa, Hafidh Saleh, Meneja, Daktari Edward Bavu, Jacob Onyango, Mchua Musuli na Mohamed Omar ‘Mpogolo’, kama Msimamiza wa Zana za Kikosi.
Akiongea mara baada ya Hafla hiyo ya Utambulisho, Lwandamina alisema: "Ni changamoto mpya kwangu, naijua Yanga ni Klabu kubwa lakini nitahakikisha natumia kila linalowezekana kuhakikisha tunafanya vizuri katika Ligi na michuano ya Kimataifa.
Lwandamina anategemewa kuanza kazi yake rasmi mara moja kutayarisha Kikosi kwa ajili ya Mzunguko wa Pili VPL ambao utaanza Desemba 17
VPL
Msimamo – Timu za Juu:
1 Simba Mechi 15 Pointi 35
2 Yanga Mechi 15 Pointi 33
3 Azam Mechi 15 Pointi 25
4 Kagera Mechi 15 Pointi 24
5 Mtibwa Mechi 15 Pointi 23
Mzunguko wa Pili
Round 16
|
17.12.2016(Sat)
|
121
|
JKT RUVU
|
Vs
|
YOUNG AFRICANS
|
MAIN NATIONAL STADIUM
|
DAR ES SALAAM
|
||
17.12.2016(Sat)
|
122
|
MBEYA CITY
|
Vs
|
KAGERA SUGAR
|
SOKOINE
|
MBEYA
|
|||
17.12.2016(Sat)
|
123
|
NDANDA FC
|
Vs
|
SIMBA SC
|
NANGWANDA
|
MTWARA
|
|||
17.12.2016(Sat)
|
124
|
MWADUI FC
|
Vs
|
TOTO AFRICAN
|
MWADUI COMPLEX
|
SHINYANGA
|
|||
17.12.2016(Sat)
|
125
|
MBAO FC
|
Vs
|
STAND UNITED
|
CCM KIRUMBA
|
MWANZA
|
|||
17.12.2016(Sat)
|
126
|
RUVU SHOOTING
|
Vs
|
MTIBWA SUGAR
|
MABATINI
|
COAST REGION
|
|||
18.12.2016(Sun)
|
127
|
AFRICAN LYON
|
Vs
|
AZAM FC
|
KARUME
|
DAR ES SALAAM
|
|||
18.12.2016(Sun)
|
128
|
TANZANIA PRISONS
|
Vs
|
MAJIMAJI FC
|
SOKOINE
|
No comments:
Post a Comment