EPL, Ligi Kuu England,ipo tena dimbani na Jumamosi zipo Mechi 6 lakini Bigi Mechi ni ile ya Stamford Bridge kati ya Wenyeji Chelsea na Tottenham Hotspur.
Mechi ya Kwanza Jumamosi ni kati ya Burnley na Manchester City na hiyo ni nafasi safi kwa City kutwaa uongozi wa EPL kutoka Nafasi ya 3 dhidi ya Burnley ambayo ipo ya 12.Wakishinda, City watakuwa na Pointi 30 na kuwazidi Vinara Chelsea ambao wana Pointi 27 na wanacheza baadae hiyo Jumamosi, ikiwa ni Mechi ya mwisho ya Siku hiyo, kwenye Dabi ya Jiji la London dhidi ya Spurs ambao wako Nafasi ya 5 na wana Pointi 24.
Kati ya Mechi hizo za Kwanza na za Mwisho hiyo Jumamosi zipo Mechi 4 na moja ni ile ya huko Anfield ambapo Liverpool, ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 27, watacheza na Sunderland ambao wako Nafasi ya Pili toka mkiani.
Jumapili zipo Mechi 4 lakini macho ya Wadau wengi ni huko Emirates Jijini London na Old Trafford Jijini Manchester wakati Arsenal, walio Nafasi ya 4, watacheza na Bournemouth walio Nafasi ya 10 huku Man United, ambao ni wa 6, wataivaa Timu ya 17 West Ham United.
EPL - LIGI KUU ENGLAND
Ratiba:
**Saa za Bongo
Jumamosi Novemba 26
1530 Burnley v Manchester City
1800 Hull City v West Bromwich Albion
1800 Leicester City v Middlesbrough
1800 Liverpool v Sunderland
1800 Swansea City v Crystal Palace
2030 Chelsea v Tottenham Hotspur
Jumapili Novemba 27
1500 Watford v Stoke City
1715 Arsenal v Bournemouth
1930 Manchester United v West Ham United
1930 Southampton v Everton
Jumamosi Desemba 3
1530 Manchester City v Chelsea
1800 Crystal Palace v Southampton
1800 Stoke City v Burnley
1800 Sunderland v Leicester City
1800 Tottenham Hotspur v Swansea City
1800 West Bromwich Albion v Watford
2030 West Ham United v Arsenal
Jumapili Desemba 4
1630 Bournemouth v Liverpool
1900 Everton v Manchester United
Jumatatu Desemba 5
2300 Middlesbrough v Hull City
No comments:
Post a Comment