Makamu
wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali inajipanga
kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye viwanda kama hatua
ya kuviwezesha viwanda vingi nchini kuongeza uzalishaji na kutoa ajira
nyingi kwa watanzania.
Samia ametoa kauli hiyo jana Jijini Arusha baada ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Mount Meru Millers ili kujua changamoto zinazokikabili kiwanda hicho ili Serikali iweze kuzifanyia kazi katika kuleta unafuu kwenye uzalishaji wa mafuta ya kupikia nchini.
Alisema
mlolongo wa kodi zinazotozwa kwa wamiliki wa viwanda hazina uratibu
mzuri hivyo mkakati ya Serikali wa awamu ya Tano inataka kuweka
utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi hizo ikiwemo kuondoa kodi ambazo ni
kero kwenye viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Mount Meru Millers Atul Mittal alisema
kama Serikali itafuta au kuondoa utitiri wa kodi wanazotozwa kwenye
viwanda hivyo watakuwa na uwezo wa kuongeza maradufu uzalishaji na kutoa
ajira nyingi kwa Watanzania.
No comments:
Post a Comment