Makamu
wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa
serikali imeweka mipango na mikakati thabiti ya kukabiliana na idadi
kubwa ya vifo vinasababishwa na saratani hasa saratani ya matiti na
mlango wa kizazi kote nchini.
Ametoa
kauli hiyo jana katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza wakati
akizundua kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mabadiliko ya
awali ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Mwanza.
Samia
alisema Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo Kusini mwa Jangwa la Sahara ina
kiwango cha juu cha vifo vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi
ambapo asilimia 60 ya vifo vyote vinavyotokea Kusini mwa jangwa la
Sahara vinasababishwa na saratani hiyo.
Makamu
wa Rais alisema kuwa vifo vingi vinatokana na uelewa mdogo, imani
potofu, gharama kubwa za matibabu, unyanyapaa na kuwepo kwa vituo
vichache wa kufanyia uchunguzi hapa nchini ambapo kwa sasa tiba ya
mionzi inapatikana katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dar es
Salaam.
Katika
kukabiliana na tatizo hilo, Makamu wa Rais alisema kuwa Wizara ya
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea kiasi cha
shilingi bilioni Tano kutoka Benki ya Dunia fedha ambazo zitawezesha
vituo Vitatu kwa kila Halmashauri ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za
uchunguzi na matibabu ya mapema ili wanawake kote nchini hasa wale wale
wa vijijini waweze kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa ukaribu kwenye
maeneo wanayoishi.
“Wote
ni mashuhuda kwa namna saratani ya mlango wa kizazi inavyosababisha
vifo vingi hali ambayo hutokana na magonjwa wanaogundulika na ugonjwa
kuwa tayari wamefikia hatua isiyotibika na kwa pamoja saratani hizi
mbili husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akinamama”
Makamu
wa Rais alisisitiza kuwa kwa sasa tayari kuna vituo takribani 300
vinavyotoa huduma za upimaji wa dalili za awali katika vituo vya afya
kote nchini na hivyo vituo vipya vitaongeza huduma endelevu ili
kupunguza vifo vitokanavyo na saratani.
Kwa
upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye
wagonjwa wengi wa saratani ya mlango wa kizazi na pia ndiyo inaongoza
katika nchi za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment