MEYA KALISTI LAZARO AWATAKA WANAHABARI KUTOTUMIKA VIBAYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, November 20, 2016

MEYA KALISTI LAZARO AWATAKA WANAHABARI KUTOTUMIKA VIBAYA


ANDREA NGOBOLE


Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) Andrew Ngobole akizungumza katika Mahafali ya Chuo hicho ambapo Wanafunzi wametunukiwa vyeti vya Shahada na Stashahada.Picha na Ferdinand Shayo

Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC)  Joseph Mayagila akizungumza katika Mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo,wapili kutoka kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro,wakwanza kushoto ni Diwani wa kata ya Themi ,Melans Kinabo na kulia ni Mkurugenzi wa Safina Radio Elifuraha Samboto Picha na Ferdinand Shayo
Picha na Ferdinand Shayo

Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akimtunuku cheti cha stashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji Amani Mmbando wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC),wawatu kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC)  Joseph Mayagila.Picha na Ferdinand Shayo


Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akimtunuku cheti cha stashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji  ANASTAZIA ELIASI wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC),wawatu kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC)  Joseph Mayagila.Picha na Ferdinand Shayo


Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akikabidhiwa Zawadi na Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC)  Joseph Mayagila katika Mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo.Picha na Ferdinand Shayo
Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro akizungumza katika Mahafali ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  Arusha (AJTC) ,Kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo hicho Joseph Mayagila,kushoto ni Diwani wa kata ya Themi ,Melans Kinabo.Picha na Ferdinand Shayo
 Mkuruf=gezi mtendaji wa mafunzo wa AJTC akitoa hotuba ya katika mahafali hayo na kumkaribisha mgeni rasmi ili aweze kuwatunuku vyeti wahitimu
Wahitimu wa chuo hico wakirusha kofia juu na kushangilia mara baada ya kutunukiwa diploma ya uandishi wa habari ya chuo cha uandishi wa habari Arusha

picha ya pamoja na wahitimu






Na Ferdinand Shayo,Arusha .


Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro amewataka wanahabari nchini kuhakikisha wanatumikia jamii masikini isiyosikika ili kuikwamua na matatizo yanayoikabili.
ameyasema hayo alipokuwa akiwatunuku diploma ya uandishi wa habari zaidi ya wahitimu 50 waliohitimu katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji  (AJTC) huku akiwataka kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za jamii na kuleta mabadiliko kupitia kalamu zao.


Kalisti amewataka Wanahabari kujikita katika kuandika habari za kijamii zitakazosaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kuleta suluhu kwenye matatizo ya jamii.


Aidha kutokana na kupitishwa kwa sheria mpya ya habri Ameishauri serikali kuangalia upya mswada wa habari na kuufanyia marekebisho katika vipengelea ambavyo vinaminya haki ya habari.


Naye Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji ,Joseph Mayagila amesema kuwa tasnia ya habari ni tasnia muhimu katika kuchochea maendeleo ya nchi kwani bila taarifa hakuna maendeleo.


Alisema kuwa ni vyema serikali ikatazama upya utekelezaji wa sheria mpya na kufanyia kazi mapungufu ili wanahabari waendelee kuwahabarisha Watanzania.

No comments:

Post a Comment