e headline"> “Sitachukua hata Dola moja kwenye mshahara wa Urais”, ni kauli ya Rais mteule Donald Trump baada ya kuulizwa kwamba atakuwa akiufanyia nini mshahara wa Dola laki nne (400,000 kwa mwaka) ambazo ni mshahara wa Rais wa Marekani anapokuwa Ikulu ya White House.
Kauli
hii aliitoa Donald Trump mshindi wa kiti cha Urais nchini Marekani
wakati akiwa kwenye kampeni zake September 17, 2015, huko Rochester, New
Hampshire: “Kitu cha kwanza
ninachotaka kuwaambia na nitakifanya kama nikichaguliwa kuwa Rais,
Sitakuwa nikichukua mshahara, hata dola moja siihitaji, hicho sio kitu
kikubwa kwangu.” – Donald Trump
Kwa
mujibu ripoti mpya zilizotolewa na jarida la watu maarufu duniani
Forbes, limetaja utajiri wa Rais huyo mteule kuwa unafikia Dola Bilioni
3.7 za Marekani ambazo ni zaidi ya shilingi Trilioni 8 za Tanzania
Katika
Video hapa chini, Donald Trump anasikika akisema kwamba alikuwa
akijigharamia kwa fedha yake mwenyewe wakati wa kampeni zake, hivyo
hatachukua mshahara wake zaidi ya kupokea vitu vidogo ambavyo ni vya
lazima akiwa Rais.
No comments:
Post a Comment