UEFA CHAMPIONZ LIGI: REAL, MONACO, LEICESTER, LEVERKUSEN, JUVE, ZASONGA! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 23, 2016

UEFA CHAMPIONZ LIGI: REAL, MONACO, LEICESTER, LEVERKUSEN, JUVE, ZASONGA!



UEFA CHAMPIONZ LIGI
Mechi za 5 za Makundi
Jumanne 22 Novemba 2016
KUNDI E
CSKA Moscow 1 Bayer 04 Leverkusen 1           
Monaco 2 Tottenham Hotspur 1
KUNDI F
Borussia Dortmund 8 Legia Warsaw 4             
Sporting Lisbon 1 Real Madrid 2            
KUNDI G
FC Copenhagen 0 FC Porto 0                
Leicester City 2 Club Brugge 1
KUNDI H
Dinamo Zagreb 0 Lyon 1            
Sevilla 1 Juventus 3         
++++++++++++++++++++++++++++
KWENYE Mechi 8 za Makundi E hadi H ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, zikiwa ni Mechi za 5 za Makundi Monaco, Bayer Leverkusen, Real Madrid. Leicester City na Juventus zimetinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 hapo Jana huku wakibakisha Mechi 1 mkononi.UCL-NOV22-E-F
Mabingwa Watetezi Real Madrid, wakicheza Ugenini huko Lisbon, Ureno, waliichapa Mtu 10 Sporting Lisbon 2-1 na kufuzu.
Real walitangulia kufunga katika Dakika ya 29 kupitia Raphael Varane na Sporting kubaki Mtu 10 katika Dakika ya 64 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Jao Pereira.
Lisbon walisawazisha Dakika ya 80 kwa Penati ya Adrien Silva lakini Dakika ya 87 Karim Benzema, alietoka Benchi, akafunga Bao la Pili na la ushindi.
Real sasa wamefuzu kutoka Kundi F pamoja na Borussia Dortmund ambao Jana waliinyuka Legia Warsaw 8-4 na Mechi ya mwisho kati ya Real na Dortmund ndio itaamua nani Mshindi wa Kundi hili.
++++++++++++++++++++++++++++
Timu 10 ambazo zimefuzu – Bado 6:
-Arsenal, Paris St Germain, Atletico Madrid, Bayern Munich, Borussia Dortmund, Monaco, Bayer Leverkusen, Real Madrid. Leicester City, Juventus
Timu ambazo zimetupwa nje ya Mashindano:
- Ludogorets, Basel, PSV Eindhoven, FC Rostov, Club Brugge, Dinamo Zagreb, Legia Warsaw, Tottenham, CSKA Moscow, Sporting Lisbon
++++++++++++++++++++++++++++
Nao Mabingwa wa England Leicester City, wakicheza UCL yao ya kwanza kabisa, wamefanikiwa kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku wakiwa na Mechi 1 mkononi baada ya kuifunga Club Brugge 2-1 kwa Bao za Shinji Okazaki na Penati ya Riyad Mahrez huku Brugge wakifunga Bao lao kupitia Jose Izquierdo.
Timu nyingine ya England, Tottenham Hotspur, wakiwa Kundi E, wametupwa nje ya Mashindano kwa kuchapwa 2-1 na AS Monaco ambao sasa wamefuzu.
Huko Spain, waliokuwa Vinara wa Kundi H Sevilla, ambao kwa Misimu Mitatu iliyopita ni Mabingwa wa UEFA EUROPA LIGI, wametwangwa 3-1 na Juventus ambao sasa wamefuzu.
Sevilla walitangulia kufunga kupitia Nicolas Pareja na Juve kujibu kwa Penati ya Claudio Marchisio na Bao za Leonardo Bonucci na Mario Mandzucic.
Hii Leo Mechi za Makundi a hadi D zitachezwa na Vigogo Barcelona, walio Ugenini na Celtic, na Manchester City, ambao wako Ugenini na Borussia Moenchengladbach, wanaweza kufuzu kwa ushindi.
UCL-NOV21-A-DUEFA CHAMPIONZ LIGI
Ratiba Mechi za 5 za Makundi
***Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa
Jumatano 23 Novemba 2016
KUNDI A
Arsenal v Paris Saint Germain               
Ludogorets Razgrad v FC Basel             
KUNDI B
2045 Besiktas v Benfica              
Napoli v Dynamo Kiev                
KUNDI C
Bor Monchengladbach v Manchester City
Celtic v Barcelona
KUNDI D
2000 FC Rostov v Bayern Munich           
Atlético Madrid v PSV Eindhoven           
Ratiba Mechi za 6 na za mwisho za Makundi
***Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
Jumanne 6 Desemba 2016
KUNDI A
FC Basel v Arsenal
Paris Saint Germain v Ludogorets Razgrad                
KUNDI B
Benfica v Napoli               
Dynamo Kiev v Besiktas             
KUNDI C
Barcelona v Borussia Monchengladbach           
Manchester City v Celtic
KUNDI D
Bayern Munich v Atlético Madrid           
PSV Eindhoven v FC Rostov                  
Jumatano 7 Desemba 2016
KUNDI E
Bayer 04 Leverkusen v Monaco             
Tottenham Hotspur v CSKA Moscow                
KUNDI F
Legia Warsaw v Sporting Lisbon           
Real Madrid v Borussia Dortmund         
KUNDI G
Club Brugge v FC Copenhagen              
FC Porto v Leicester City
KUNDI H
Juventus v Dinamo Zagreb         
Lyon v Sevilla         
++++++++++++++++++++++++++++
TAREHE MUHIMU:
MECHI ZA MAKUNDI:
Mechi ya Kwanza: 13 na 14 Septemba
Mechi ya Pili: 27 na 28 Septemba
Mechi ya Tatu: 18 na 19 Oktoba
Mechi ya Nne: 1 na 2 Novemba
Mechi ya Sita: 22 na 23 Novemba
Mechi ya Sita: 6 na 7 Desemba
MECHI ZA MTOANO:
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)

No comments:

Post a Comment