Mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme alilazimika kusimama mbele ya umati wa watu katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa ya moyoni baada ya kusikia simulizi ya mwanafunzi Joyce Samwel aliyefanyiwa kitendo cha ubakaji na mwalimu wake hadi kumsababishia kukatisha masomo yake..
‘Inasikitisha
kuona ubakaji unaendelea kwa kasi, ukatili ndani ya jamii unaendela kwa
kasi, takwimu za ukatili wa kijinsia zimekuwa zikiongezeka mwaka hadi
mwaka ambapo mwaka 2014 mauaji yalikuwa 134, ubakaji kesi 181, ulawiti
kesi 30 na jumla ni kesi 345‘ –DC Joyce Mndeme
‘Takwimu hizi zimeendelea
kupanda na mwaka 2015 kesi za mauaji zilikuwa 143, ubakaji kesi 173,
ulawiti kesi 40 na kunajisi kesi 4 jumla kesi 360 huu ni ukatili mkubwa
sana‘ –DC Joyce Mndeme
‘Hadi
kufikia mwezi wa kumi mwaka huu kuna kesi 108 za mauaji, ukabaji 135,
ulawiti kesi 31, kunajisi 4, kutupa watoto zilizoripotiwa zipo kesi 2
jumla kesi 983 ni kesi nyingi sana na zinahuzunisha kwasababu matendo
haya yanafanyika miongoni mwa jamii zetu‘ –DC Joyce Mndeme
‘Tumeusikiliza
ushuhuda wa Joyce naamini kila mtu kaguswa katika hili, ndugu zangu
mfano wa Joyce ni sehemu tu na ukatili kama huu upo mwingi inasikitisha
sana tena kufanyiwa na mwalimu ambaye ni mzazi wake wa pili, ndioto za
Joyce zimeishia njiani kwa kubakwa‘- DC Joyce Mndeme
‘Serikali tumeguswa na tatizo hili na tunaahidi kulishughulikia kwa ukamilifu na hatimaye ndoto za Joyce zitafanikiwa‘- DC Joyce Mndeme
Unaweza kuendelea kumsikiliza DC Joyce Mndeme kwenye hii video hapa chini….
No comments:
Post a Comment