November 25 umefanyika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo kwa Dodoma yalifanyika katika viwanja vya Nyerere square huku mgeni rasmi akiwa ni mkuu wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme.
Moja ya tukio lililogusa hisia za wengi ni simulizi ya mwanafunzi Joyce Samwel aliyebakwa na mwalimu wake na kisha kumsababishia ujauzito uliopelekea kukatisha masomo yake..
‘Nilipofika
darasa la saba mwalimu Mtajama aliniita ofisini kwake akaniambia
ananipenda nikamkatalia na kumwambia mimi nataka kuendelea na masomo
akaniambia kama ni kusoma shule nitasomatu‘- Joyce Samwel
‘Nikamuuliza je, nikipata
mimba itakuwaje akaniambia nisiwe na wasiwasi nikipata ujauzito
tutalitatua, siku ya pili aliniita nyumbani kwake na nilivyoenda
akanivuta chumbani kwake na kunivua sketi‘ –Joyce Samwel
‘Baadae
alinilaza kwenye kitanda chake na kuniingilia kimwili na baadae
nikapata ujauzito, nilivyomtaalifu akasema ataongea na wazazi wangu
hivyo nisiwe na wasiwasi‘ –Joyce Samwel
Unaweza kuendelea kumsikiliza kwenye hii video hapa chini…..
No comments:
Post a Comment