Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini Kenya (COTU), Bw.
Francis Atwoli amesema anaikubalia kasi ya Rais Magufuli katika
kupambana na rushwa.
Pia
amewataka Watanzania wamuunge mkono badala ya kulalamikia kasi kwani
wao wanatamani mwakani aende kugombea kwao katika uchaguzi mkuu ujao.
Ametoa
kauli hiyo jana katika Mkutano Mkuu wa Sita wa Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) katika ukumbi wa Mwalimu Julius K. Nyerere
ulioko Chuo cha Mipango, nje kidogo ya mji wa Dodoma, uliofunguliwa na
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
“Ninawasihi
wanaTUCTA suala la rushwa msilipe nafasi. Mpambane nayo kwa sababu kule
kwetu imeota mizizi. Muungeni mkono Rais Magufuli, badala ya kulalamika
kuwa kasi yake ni kubwa mno. Mnasema eti ana spidi sana, mkiona taabu
mtuazime japo kwa mwaka mmoja ili aje atunyooshee mambo kule kwetu,” alisema huku akishangiliwa.
Aliwataka
wahimize uhusiano uliopo baina ya vyama vya wafanyakazi, waajiri na
Serikali iliyopo madarakani na kuwataka wadumishe umoja miongoni mwa
viongozi na wanachama mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment