
Mwanafunzi
wa kidato cha pili wa shule ya sekondari Mringa, Vanessa Josephat [16]
mkazi wa Sakina jijini hapa amejeruhiwa vibaya kwa kupigwa risasi
kichwani na walinzi wa kampuni ya ulinzi ya kifaru waliokuwa wakiwatoa
kwa nguvu kwenye nyumba yao yenye mgogoro .
Tukio
hilo limethibitishwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Arusha
Charles Mkumbo ambaye alisema kuwa polisi inamshikilia Fabian Charles
mlinzi wa kampuni ya kifaru pamoja na silaha aina ya shoot gun iliyo
tumika katika tukio hilo huku majeruhi amelazwa katika hospitali ya KCMC
kutokana na hali yake kuwa mbaya .
Kamanda
mkumbo alisema kuwa tukio hilo limetokea jana majira ya saa tatu
asubuhi katika eneo la sakina jijini hapa, ambapo alisema walinzi watatu
wa kampuni hiyo waliokuwa wakilinda nyumba hiyo inayomilikiwa na
Josephat Nehemia walitumia silaha hiyo kuwafyatulia familia inayoishi
hapo ili waondoke na ndipo silaha hiyo ilipomjeruhi mwanafunzi huyo .
Taarifa
zinaeleza kuwa December 21 mwaka huu kampuni ya udalali ya Marc
Recorders Limited wakiwa na mabaunsa na watu wengine walivamia nyumba
hiyo na kuwatoa nje wamiliki wa nyumba hiyo na kuondoka na vyombo vyao
vya ndani wakidai nyumba hiyo imeshauzwa kwa , Thobias Ludovick Senya
baada ya mmiliki kushindwa kulipa deni la shilingi million 3.7 alilokuwa
akidaiwa na taasiai ya fedha Heritage.
Baada
ya tukio hilo familia hiyo yenye watu wapatao kumi wakiwemo watoto na
kichanga walianza kulala nje kando ya geti la nyumba hiyo wakipigwa na
baridi kali pasipo kuwa na msaada wowote
Mmiliki
wa nyumba hiyo Josephat Nehemia Ogaga alisema baada ya familia yake
kutolewa nje wakati yeye akiwa safarini walikuja walinzi hao wa kampuni
ya kifaru na kuanza kulinda na baada ya yeye kurejea alifanikiwa
kuwaondoa walinzi hao na kuirejesha ndani familia yake akidai taratibu
za kuuza nyumba yake hazikufuatwa ila kilichofanyika ni uhuni .
“Nikweli
nilikuwa nadaiwa na Heritage financial shilingi milioni 3 .7 na
nililipa deni na kubaki shilingi million 1.8 hivyo hatua ya kuja kuuza
nyumba yangu yenye thamani shilingi million 200 kwa deni hilo ni uhuni
mtupu umefanyika” alisema Nehemia
Hata
hivyo siku moja baadae walinzi hao walirejea tena wakiwa na silaha za
moto na kuanza kufyatua risasi ovyo ndani ya nyumba hiyo kwa lengo la
kuwatisha familia hiyo ili waondoke ndani ya nyumba hiyo ambapo moja ya
risasi ilimjeruhi mwanafunzi huyo kichwani ambaye amelazwa katika
hospitali ya rufaa ya KCMC Mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matibabu
Kamanda
Mkumbo amezitaka kampuni za ulinzi kutoingilia migogoro bila kufuata
utaratibu kwani vyombo vyenye mamlaka ya kushughulikia migogoro kama
hiyo vipo na hivyo amezitaka kampuni za ulinzi kufuata taratibu zao za
utendaji wa kazi na kuacha kukimbilia maslahi yao ya kupata fedha
haraka,
Mkumbo alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
No comments:
Post a Comment