Watu
wote waliokuwa wamefanya usaili kwa ajili ya ajira serikalini kupitia
Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma kabla ya ajira kusimamishwa,
watafutwa ndani ya miezi 6 na kulazimika kuomba upya kipindi ajira hizo
zitakapotangazwa tena.
Hilo
limebainishwa na sekretarieti hiyo kupitia majibu kwa wadau mbalimbali
kwa mwezi Desemba ambao wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa kila
mwezi kupitia tovuti yake, na kubainisha kuwa suala hilo litawahusu wale
ambao walifaulu usaili lakini kabla hawajapangiwa vituo vya kazi au
kupewa barua na waajiri wao, ajira zikasimamishwa ili kupisha uhakiki wa
watumishi hewa.
Taarifa
hiyo imesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa sekretarieti hiyo,
kwamba majina ya waliofaulu huhifadhiwa kwenye kanzi data (Database) kwa
muda usiozidi miezi sita, na baada ya hapo majina hayo hufutwa.
"Kwa
mujibu wa Taratibu zetu za uendeshaji wa mchakato wa ajira majina ya
waombaji kazi waliofaulu lakini hawakupangiwa vituo vya kazi kwa sasa
huhifadhiwa kwenye kanzi data kwa muda usiozidi miezi sita" Imesema taarifa hiyo
Kwa
kuwa ajira zilisitishwa mwezi Juni, na sasa ni mwezi Desemba, utaratibu
huo unamaanisha kuwa wasailiwa wote waliofaulu lakini hawakupangiwa
kazi, watalazimika kusubiri upya matangazo ili waombe upya na kufanya
usaili upya.
Aidha
Sekretariet hiyo imebainisha kuwa zoezi ya uhakiki wa watumishi hewa
bado linaendelea, na kwamba wakipewa ruhusa ya kutangaza ajira wakati
wowote watatangaza.
No comments:
Post a Comment