Wakati macho na masikio ya Watanzania wakisubiri kusikia hatma ya
wasanii wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya, wasanii wanne
waliofika Kituo Kikuu cha Polisi bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa
mahojiano zaidi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema
kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed (TID), na
mtangazaji maarufu wa Clouds TV Babuu wa Kitaa bado wanashikiliwa na
jeshi hilo.
“Bado tunawashikilia kwa mahojiano zaidi,” amesema Sirro kwa kifupi.
Wasanii wengine waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda ambao wanatakiwa kufika kituoni Jumatatu ni Vanessa Mdee, Tunda
na watu wengine Halidali Kavila, Amani, Kashozi na Omry Sanga.
No comments:
Post a Comment