Kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho ameongeza mkataba wa muda mrefu na klabu hiyo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
Taarifa zinasema Mbrazil huyo, amesaini
mkataba utakaomuweka Anfield hadi mwaka 2022, huku kukiwa hakuna
kipengele cha kumwachia mchezaji huyo.
Mara baada ya kusaini mkataba huo, Coutinho amesema kuwa anawashukuru watu wote wa Liverpool, na kuahidi kuitumikia klabu hiyo kwa nguvu zake zote, ili kulipa thamani anayopewa na klabu hiyo.
Coutinho aliyetoka kuuguza majeraha ya kifundo cha mguu kwa mwezi mmoja na nusu hadi sasa ameifungia klabu yake mabao 6, katika michezo 18, kwenye msimu huu.
No comments:
Post a Comment