MWANADADA anayetamba na ngoma ya ‘Shindu’ Mwaga Maji Tucheze Kama Kambare, Snura Mushi (pichani) ameeleza kiu yake ya kutaka kufanya kazi na mwanadada mwenzake Zuwena Mohammed ‘Shilole’ endapo atakuwa tayari.
Snura amebainisha hayo usiku wa Jumanne,
Januari 24, 2017 wakati akijibu swali kwenye interview ya kipindi cha
Redio EFM. Snura amesema kuwa kwa sasa hana bifu kabisa na Shilole,
hayo yalikuwa mambo ya zamani na yalisha kwisha kitambo na endapo
ikitokea nafasi ya wawili hao kukaa chemba na kufanya kazi pamoja yuko
tayari kwa asilimia zote.
Shilole
“Kwa sasa sina bifu lolote na
Shilole, tuko sawa, hayo yalikuwa mambo ya zamani sana tulishayamaliza,
tupo sawa. Muziki wake na wangu uko tofauti hatuwezi kugombana”
“Kwanza natamani sana kufanya kazi
pamoja na Shilole, ikiwezekana tufanye wimbo wa pamoja au movie (filamu)
kwa kuwa yeye ni msanii mzuri wa kuigiza naamini tukifanya hiyo
tutatengeneza pesa nzuri mimi na yeye”
“Kingine ni kwamba natamani pia
kufanya naye shoo moja jukwaani hata kama ni hapa Dar es Salaam au
popote, kwa maana sisi wasanii tupo kwa ajili ya kutafuta pesa, kwa hiyo
ikitokea nafasi kama hiyo itakuwa poa sana.” Alisema Snura.
Shilole
Mbali na hayo Snura hakusita kueleza
jitihada zake za kumtafuta Shilole licha ya yeye kuonekana kama hayuko
tayari kufanya hivyo.
“Nimewahi kumtafuta kwa jitihada
zangu ili tuweze kufanya angalau jambo moja kati ya hayo (shoo, wimbo au
filamu) lakini inavyoonekana mwenzangu kama hayuko tayari.” Alimalizia Shilole.
No comments:
Post a Comment