Kutoka Mahakamani kwenye kesi ya rushwa kwenye soka ya ile sauti iliyosambaa - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, January 25, 2017

Kutoka Mahakamani kwenye kesi ya rushwa kwenye soka ya ile sauti iliyosambaa


Mashaidi watatu 3 kwa upande wa Jamhuri wa kesi inayohusishwa na upangaji wa matokeo pamoja na rushwa kwenye michezo ya  ligi daraja la kwanza msimu uliyopita, wamewasilisha ushahidi wao katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam.

Kesi hiyo ambayo inawahusu waliokuwa maafisa wa shirikisho la soka TFF Juma Matandika pamoja na Martin Chacha aliyekua mkurugenzi wa mashindano ilianza kusikilizwa mwishoni mwa mwaka 2016.

Miongoni mwa mashaidi waliowasilisha utetezi wao ni pamoja na  mwenyekiti wa timu ya Geita Gold Sports Leonard Bugomola na kuthibitisha kuwa ile sauti iliyorekodiwa na kusambaa mtandaoni ilikuwa ni kweli.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi January 27 2017 saa 5 asubuhi.

 

No comments:

Post a Comment