Upande
wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal
Malinzi na wenzake umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itoe
maelekezo mahususi kwa upande Serikali kuharakisha upelelezi, kinyume na
hapo Mahakama iwasikilize na iwaachiwe.
Wakili
wa utetezi, Domician Rwegoshora amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilfred
Mashauri kwamba wanautaka upande wa mashtaka uharakishe upelelezi kwa
sababu kesi hiyo haina dhamana, hivyo washtakiwa wakiendelea kukaa ndani
wanateseka.
"Mahakama
itoe maelezo mahususi kwa upande wa mashtaka kwa muda mfupi, au
washtakiwa wasikilizwe ikiwezekana Mahakama iwaachie.” Amesema Wakili
Domician Rwegoshora.
Baada
ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali, Vitalis akaeleza kuwa upelelezi
upo katika hatua ya mwisho na muda si mrefu itaanza kusikilizwa.
No comments:
Post a Comment