
Waziri
wanchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleman Jafo
amezindua rasmi kampeni ya uanzishaji wa viwanda vidogo na vya kati kila mkoa
kwa lengo la kuinua uchumi wa nchi ifikapo 2020.
Uzinduzi
huo umefanyika Mjini Dodoma ambapo waziri TAMISEMI Sememani Jafo amesema lengo
hilo litafanikiwa endapo watendaji wake watafanya kazi kwa weledi na kusema
kuwa wizara yake itaandaa mazingira
rafiki yatakayowezesha utekelezaji wa azma hiyo.
Waziri
wan chi ofisi ya waziri mkuu anayesimamia sera ,bunge kazi ajira na wenye
ulemavu Jenista Mhagama,amesema serikali imejipanga kuwajengea wananchi
ujuzi wa kuingia katika uchumi wa viwanda.
Kaulimbiu
ya kampeni ya uanzishwaji wa viwanda 100 kila mkoa inasema,mkoa wetu,viwanda
vyetu.
Hii
ni baada ya kutolewa maagizo ya serikali kuhusu uanzishwaji wa viwanda 100
vidogo na vya kati kila mkoa ,ambapo uzinduzi wa kampeni hiyo umefanyika
rasmi kitaifa.
No comments:
Post a Comment