WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii wote kutekeleza wajibu wao wa
msingi kwa kuhakikisha watoto wanalindwa dhidi ya vitendo vya ukatili wakiwa
shule na nje ya shule.
Taarifa ya utafiti wa hali ya afya ya uzazi ,mtoto na malaria ya
mwaka 2015/2016 inaonyesha kuwa asilimia 27 ya watoto wakike wanapata mimba
wakiwa na umri chini ya umri wa miaka 18..
Tatizo hili lipo zaidi mikoa ya Katavi (asilimia 45),Tabora
(asilimia 43),Dodoma (asilimia 39), Morogoro (asilimia 39) na mkoa wa mara
(asilimia 37)
Akizungumza leo mjini Dodoma wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu
wa 12 wa sekta ya maendeleo ya jamii Waziri Ummy amesema kuwa kupitia mkutano
huo maafisa maendeleo ya jamii amesema kuwa kupitia mkutano huo maafisa
maendeleo ya majii wanatakiwa wanatoka na mikakati madhubuti ya kudhibiti
vitendo vya ukatili katika jamii.
Naye Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Sihaba Nkinga amesema kuwa katika awamu ya sasa Wataalamu wa Maendeleo ya Jamii
wana wajibu wa kuelimisha na kuhamsha ari ya wananchi kufanya kazi za
uzalishaji ambapo hapa anabainisha baadhi ya mada zitakazojadiliwa
Kwa upande wake mkurugenzi wa maendeleo ya jamii tika wizara ya
afya maedeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, idara kuu ya maendeleo ya
jamii Patrick Golwike amesema kuwa wao kama maafsa maendeleo ya jamii
wanatakiwa kutambua majukumu yao.
Takwimu za elimu kwenye shule za msingi kwanzia mwaka 2011 hadi
2015 zinaonyesha kuwa wasichana elfu 39,243 waliacha shule kutokana na sababu
mbalimbali na wasichana elfu 3,806 walikatishwa masomo yao kwasababu ya mimba.
Kutokana na hayo maafisa maendeleo ya jamii anawataka kufuatilia
mwenendo wa taarifa zitakazotolewa na wakuu wa shule ili kubaini ukubwa wa
tatizo katika halmashauri kwa lengo la kubuni na kupanga mbinu za kukabiliana
na tatizo hilo kwa watoto walio shuleni.
No comments:
Post a Comment