
Klabu ya Borussia Dortmund imeamua kumuweka nje kwa muda usiojulikana mshambuliaji wao tegemezi kutoka Gabon Pierre Aubameyang kwa kile kilichotajwa kama utovu wa nidhamu.
Taarifa rasmi kutoka ndani ya klabu hiyo imethibitisha kwamba Aubameyang hatakuwepo katika mchezo wa kesho ambao Borussia Dortmund wataikabili Stuttgart kutokana na matatizo hayo.
Hii sio mara ya kwanza kwa Mgabon huyu kupewa adhabu kutokana na masuala ya utovu wa nidhamu ambapo mwaka jana mwezi wa 11 aliachwa katika kikosi cha Dortmund kilichocheza zidi ya Sporting katika Champions League.
Matatizo kati ya Dortmund na Aubameyang yanaweza kuwa ishara kwamba mwanasoka huyo yuko mbioni kuachana na klabu hiyo kwani kila dirisha la usajili amekuwa akihusishwa na kuikimbia Dortmund.
Tayari katika msimu huu Aubameyang amefunga jumla ya mabao 10 lakini hajawahi kufunga tangu alipofunga katika mchezo zidi ya RB Leizpg mwezi October ambapo Borussia Dortmund walifungwa bao 3 kwa 2.
No comments:
Post a Comment