Leo hakuna habari kubwa katika soka kama habari ya Cristiano Ronaldo
kubeba tuzo yake ya 5 ya Ballon D’Or, Cr7 na Lioneil Messi ni wazi
kwamba muda wao wa kuwa bora duniani unaelekea ukingoni kwa sasa lakini
wafuatao wanaweza kuchukua nafasi zao.

1.Neymar.
Huyu ndio anapewa nafasi kubwa zaidi kuchukua utemi wa Cr7 na Messi
katika soka, tangu ahamie PSG jina lake limekuwa likizungumzwa sana na
wachambuzi wakubwa wa soka akiwemo Shaffih Dauda wanampa nafasi kuwa
mfalme wa soka.

2.Kylian
Mbappe. Kama ilivyo kwa Neymar, huyu naye anapewa nafasi kuwa mwanasoka
bora wa dunia, lakini tatizo kubwa ambalo naliona kwa Mbappe ni kivuli
cha Neymar kwani kwa sasas hata uwe na uwezo vipi lakini ukiitaja PSG
jina linalotajwa ni Neymar.

3.Harry
Kane. Nani mshambuliaji hatari zaidi duniani kwa sasa? Sina uhakika wa
moja kwa moja ni nani lakini kwa mawazo ya harakaharaka Harry Kane ni
kati ya tishio kubwa kwa sasa ulimwenguni, sio rahisi sana kuwa mchezaji
bora wa dunia ukiwa Tottenham lakini bado ana nafasi.

4.Eden
Hazard. Amekuwa imara sana na kati ya vipaji vikubwa sana katika soka
kwa sasa lakini Chelsea sio kubwa kiasi cha kumpa Ballon D’Or, kama
akihamia klabu ambayo inaweza kuchukua Champions League mara nyingi
itamuweka katika eneo zuri kuwa mkubwa zaidi.

5.Paulo
Dyabala. Anatajwa kama Messi mpya ndani ya Argentina na raia wenginwa
Argentina wana imani kubwa naye, wakati huu ambao Messi umri wake
unakwenda ni wazi kwamba itampa wigo mpana zaidi wa kuwa mchezaji mkubwa
zaidi.
No comments:
Post a Comment