MADEREVA PIKIPIKI WATAKIWA KUZINGATIA ELIMU YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZA KIZEMBE!!!!! - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, December 8, 2017

MADEREVA PIKIPIKI WATAKIWA KUZINGATIA ELIMU YA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZA KIZEMBE!!!!!



Afisa huduma na mtoa elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Dodoma Barnabas Masika amewataka wananchi wa mkoa wa Dodoma wanapo nunua chombo cha moto wafike ofisi za TRA kabla ya mwezi mmoja [siku 30] kuisha ili kubadili  umiliki.

Ameyasema hayo wakati  wa hitimisho  ya mafunzo ya elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki  yaliyo fanyika  katika kata ya Haneti  Wilayani chamwino mkoani dododma  na kuwataka wananchi wazingatie elimu wanayo pewa na wakufunzi  wao wakiongozwa na  FAUSTIN MATINA ili kuondokana na tatizo la ajali barabarani .

Pia amewaasa madereva bodaboda waliopata mafunzo na kutunukiwa vyeti wafanye utaratibu  wa malipo ili waweze kupata leseni halisi ya udereva kwa haraka.

Aidha  kwa upande wake mkuu wa kituo cha polisi cha haneti [OCS]  MOHAMED JUMA ALLY   amewaasa madereva bodaboda walio tunukiwa vyeti kupata leseni zao ili kuondoka na usumbufu barabarani  na amewataka bodaboda wengine kuiga mfano kwa wale waliopata mafunzo  na kutunukiwa vyeti na  pia kuwataka wale wote ambao hakupata mafunzo wajiunge na mafunzo hayo ili kupunguza ajali barabarani  na kusema kuwa wale wasiotaka kupata elimu hiyo  ni sawa na waahalifu   maana lengo la elimu hiyo ni kuwa na uelewa wakati wa unaendesha  pikipiki.

“lengo letu sisi polisi pamoja na wakufunzi wanaoongozwa na Faustin Matina ni kupunguza ajali za kizembe na wala sio vinginevyo na kwa wale ambao hawakushiriki mafunzo haya ni sawa na waalifu wengine tu kwa sababu sifa kubwa ya mwalifu ni kukwepa vitu vizuri na vya kimaendeleo kwa lengo la kuendelea na uhalifu wao hivyo nitapambana nao’’ Alisema Mohamedi Ally

Pamoja  na hayo Mkuu huyo wa kituo cha polisi amewataka bodaboda wote kuhakikisha kuwa wanakata leseni ndani ya muda stahiki ili kuepukana na usumbufu wawapo katika shughuli zao za kila siku.

Pia ametoa ushauri kwa wakufunzi kuwa elimu hii isiwe mwisho katika kata yake bali iwe endelevu na mwakani waje tena ila katika kipindi ambacho wakulima ndio wanatoka kuvuna kwa sababu kipindi hiki sio kizuri kwa sababu wengi wao ndio wanatayarisha mashamba kwa ajili ya kilimo hivyo wanakosa pesa kwa ajili ya kushiriki mafunzo na kupata kila kitu kinachohitajika kwa wakati.

Elimu hiyo inayotolewa na chuo cha WIDE INSTITUTE OF DRIVING chenye makao makuu yake mkoani Kilimanjaro inaendelea katika wilaya za Kondoa na Chemba mkoani Dodoma.

 HABARI PICHA 

Mkuu wa kituo cha polisi HANETI akizungumza na washiriki wa mafunzo (Picha na Okuly julius)


Afisa huduma na mtoa elimu kwa mlipa kodi mkoa wa Dodoma Barnabas Masika akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo ya usalama barabarani kata ya HANETI wilayani CHAMWINO (Picha na Okuly Julius)

Washiriki wakiwa makini kusikiliza Elimu inayotolewa

Msoma risala akiwasilisha mawazo na mapendekezo ya wenzake mbele ya mgeni rasmi.

Wahitimu wa mafunzo hayo baada ya kukabidhiwa vyeti vyao katika picha ya pamoja na wageni rasmi na watoa elimu hiyo baada ya mafunzo kufungwa.(Picha na Okuly Julius)








No comments:

Post a Comment