
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema amekwishawasilisha tamko la maadili ya
viongozi wa umma kwenye Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
tangu Alhamisi Desemba 28, 2017.
Akizungumza
na waandishi wa habari kijijini kwake Namahema ‘A’ wilayani Ruangwa
mkoani Lindi jana jioni (Ijumaa, Desemba 29, 2017), Waziri Mkuu alisema
fomu hizo zilipokelewa na amekwishapatiwa barua ya kupokea tamko hilo.
“Nimewaita
hapa ili kuthibitisha kuwa nimetekeleza takwa hilo la kisheria na
tayari Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi ya Umma imekiri kupokea tamko
langu kwa barua hii hapa,” alisema Waziri Mkuu huku akionyesha barua hiyo ambayo ilisainiwa na Jaji Harold Nsekela, Desemba 28, 2017.
“Kwa
kuzingatia mfano ulioonyesha na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ninawaagiza viongozi wote
wanaotakiwa kujaza fomu hizo kwa mujibu wa sheria wafanye hivyo na
kuziwasilisha ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017 saa 10 jioni,” alisisitiza Waziri Mkuu.
Alisema
anawakumbusha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu
Wakuu wote na viongozi wote walioko kwenye ngazi za uteuzi wahakikishe
wanatimiza takwa ambalo liko kwa mujibu wa kifungu cha 9 na cha 11 cha
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na. 13 ya Mwaka 1995.
Wakati
huohuo, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwatakia Watanzania wote heri
wakati wanaposubiri kumaliza mwaka 2017 na kuwatakia heri na fanaka
katika maeneo waliyopo wanapojiandaa kuupokea mwaka 2018.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
No comments:
Post a Comment