
Kama unavyojua, tayari ratiba ya Kombe la Shirikisho Tanzania bara (Azam Sports Federation Cup) rfaundi ya tatu tayari imeshatoka baada ya draw kuchezeshwa leo January 5, 2018.
Story kubwa ni kuhusu mtanange kati ya Green Rangers dhidi ya Singida United, hii inatokana na Warriors kuwatoa Simba mabingwa wa kombe hilo msimu uliopita. Simba walijikuta wakitupwa nje ya mashindano katika hatua ya pili ya mashindano hayo kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya kutoka sare ya kufungana 1-1.
ShaffihDauda.co.tz imepiga story na Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga kutaka kujua wamepokeaje ratiba hiyo inayowakutanisha na wababe wa Simba katika raundi ya tatu ya ASFC.
“Sisi hatuwaogopi wala hatuwahofii hao Green Warriors tena tumepokea ratiba kwa kufara kabisa kwa sababu tunajiamini kutokana na kikosi chetu hata tungepangwa na Azam wala Yanga tungecheza nao tu”-Festo Sanga, Mkurugenzi Singida United.
“Tutajiandaa kwa mchezo huo ambao tutacheza tukiwa ugenini nadhani itakuwa uwanja wa Azam Complex, uwanja huo ni mzuri na unaruhusu mpira kuchezeka.”
“Tumeingia kwenye kila kila mashindano kwa ajili ya kupambana kuchukua ubingwa, hatupo kwa ajili ya kushiriki, kocha wetu Hans van Pluijm anajua na wachezaji wanajua kwa hiyo tunataka kuchukua pia ubingwa wa kombe FA.”
“Green Warriors kuwatoa Simba kwenye mashindano haimaanishi kwamba ni wakali, isipokuwa ni matokeo ya mchezo wa soka. Kimsingi Simba ni timu kama ilivyotimu zingine na inafungika kwa hiyo kutolewa na Warriors ni sehemu ya soka.”

No comments:
Post a Comment