VIGOGO
Azam FC na Yanga SC watasafiri kwenda mikoani kumenyana na timu za
Ihefu FC na Shupavu FC katika hatua ya 32 Bora ya michuano ya Azam
Sports Federation Cup (ASFC).
Yanga
SC watakwenda Mbeya kuifuata Ihefu, mechi itakayopigwa Uwanja wa
Sokoine mjini humo, wakati Azam FC watakwenda Uwanja wa CCM Mkamba
mkoani Morogoro kumenyana na Shupavu FC.
Green
Warriors iliyowatoa mabingwa watetezi, Simba SC itaendelea kucheza
nyumbani mjini Dar es Salaam itakapowakaribisha Singida United Uwanja wa
Azam Complex, Chamazi.
Timu
ya kocha Freddy Felix Minziro, KMC itakuwa mwenyeji wa Toto mjini Dar
es Salaam, wakati Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi utahodhi mechi mbili
mfululizo za wenyeji, Kariakoo United dhidi ya washindi wa pili wa msimu
uliopita, Mbao FC ya Mwanza na Maji Maji Rangers dhidi ya Mtibwa Sugar
ya Morogoro.
Maji
Maji wataikaribisha Ruvu Shooting Uwanja wa Maji Maji mjini Songea,
Njombe Mji FC wataikaribisha Rhino Rangers Uwanja wa Saba Saba mjini
Njombe, Kiluvia United wataikaribisha JKT Oljoro Uwanja wa Mabatini,
Mlandizi mkoani Pwani na Ndanda FC watakuwa wenyeji wa Biashara United
ya Mara Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Mechi
nyingine; Pamba SC wataikaribisha Stand United Uwanja wa CCM Kirumba
mjini Mwanza, Polisi Tanzania watakuwa wenyeji wa Friends Rangers Uwanja
wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, JKT Tanzania watakuwa
wenyeji wa Polisi Dar es Salaam na Mwadui FC wataikaribisha Dodoma FC
Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga.
Tanzania
Prisons wataikaribisha Burkina Faso Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya
wakati Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Buseresere FC Uwanja wa Kaitaba
mjini Bukoba.
Mechi zinatarajiwa kucheza siku mbili mfululizo, Januari 31 na Februari 1, mwaka huu.
KMV V Toto Africans
Maji Maji v Ruvu Shooting
Njombe Mji v Rhino Rangers
Kiluvia Utd v JKT Oljoro
Ndanda Fc v Biashara United
Pamba SC v Stand United
Polisi TZ v Friends Rangers
JKT Tanzania v Polisi Dar
Ihefu FC v Yanga SC
Mwadui FC v Dodoma FC
Green Warriors v Singida United
Tanzania Prisons v Burkina Faso
Kariakoo United v Mbao FC
Maji Maji Rangers Lindi v Mtibwa Sugar
Kagera Sugar v Buseresere FC
Shupavu FC v Azam FC
No comments:
Post a Comment