Madereva wa pikipiki maarufu kama bodaboda wametakiwa kuhudhuria kwa wingi katika mafunzo ya usalama barabarani ili kupunguza tatizo la ajali pamoja na kufahamu haki zao wawapo barabarani.
Hayo yamesemwa na Mkufunzi wa mafunzo hayo BW. FAUSTIN MATINA wakati akizungumza na madereva pikipiki wa manispaa ya Dodoma na kusema kuwa mafunzo hayo yanatolew kwa kushirikiana na Ofisi ya R.T.O kupitia kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dodoma.
Aidha amesema kuwa lengo na dhumuni la mafunzo hayo ni kupunguza ajali za barabarani na kuimarisha ushirikiano kati ya jeshi la polisi pamoja na madereva pikipiki ili kufanya madereva pikipiki kujua haki zao na kufanya kazi zao kwa uhuru bila kuilaumu serikali.
Mbali na madereva bodaboda wananchi pia wametakiwa kuhudhuria mafunzo hayo kwani yanatolewa bure na kwa wale watakao fuzu vizuri mafunzo hayo watapatiwa vyeti na hatimaye kwa kushirikiana na RTO mkoa wa Dodoma watapatiwa leseni ya udereva kwa kulipa gharama za serikali tu.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza siku ya jumatatu ambapo kwa hapa Dodoma mjini yatafanyika katika Bwalo la Polisi na kule katika kata ya Veyula mafunzo hayo yatafanyika katika ukumbe wa Deo ,kwa upande wa kata ya Nzuguni yanatarajiwa kufanyika katika jengo la kata hiyo na muda wa mafunzo ni kuanzia saa nane kamili mchana mpaka saa kumi kamili jioni.
No comments:
Post a Comment