Wakati Singida United ikitarajiwa kutoa upinzani mkali dhidi ya Simba, imejikuta ikichezea kichapo cha bao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara.
Simba ikiwa imetoka kufanya vibaya kwenye mashindano ya Mapinduzi kwa kutolewa hatua ya makundi, wameishangaza Singida ambayo ilifanya kweli Mapinduzi Cup na kufika hatua ya nusu fainali huku ikiwa imepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Azam.
Singida United ilizivimbia Azam na Yanga kwenye michezo ya ligi na kuzilazimisha timu hizo kutoka sare. Walilazimishwa sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Azam kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma kabla ya kuibana Yanga na kutoka suluhu uwanja wa Namfua, Singida.
- Singida United 1-1 Azam
- Singida United 0-0 Yanga
- Simba 4-0 Singida United
Mabao hayo mawili yamemfanya Okwi kufikisha magoli 10 kwenye orodha ya wafungaji akimpiga bao Habib Kiyombo anaemfukuzia akiwa na magoli saba.
Magoli mengine ya Simba yamefungwa na Shiza Kichuya na Asante Kwasi yote yakifungwa kipindi cha kwanza.
Ushindi wa Simba dhidi ya Singida United unaifanya Simba kufikisha pointi 29 baada ya mechi 13 wakiwa mbele kwa pointi mbili dhidi ya Azam ambayo imelazimishwa sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Majimaji.
No comments:
Post a Comment