Wakazi wa Manispaa ya Dodoma wafurika katika Bwalo la Polisi kupata elimu ya usalama Barabarani. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, January 24, 2018

Wakazi wa Manispaa ya Dodoma wafurika katika Bwalo la Polisi kupata elimu ya usalama Barabarani.

Wakazi wa Manispaa ya Dodoma wamejitokeza kwa wingi kupata mafunzo ya usalama barabarani yenye lengo la kupunguza ajali barabarani.

Mafunzo hayo yanayotolewa na mkufunzi  na mkuu wa chuo cha WIDE INSTITUTE OF DRIVING kilichopo mkoani Kilimanjaro  Ndg.Faustini Matina kwa lengo la kutokomeza ajali za barabarani.

Pamoja na kutokomeza ajali hizo pia mafunzo hayo yanawajengea  madereva ujasiri wawapo Barabarani pia kujua haki zao pamoja na kuwa na uhusiano mzuri na jeshi la polisi.

Katika mafunzo hayo madereva wote watakaohitimu watapatiwa vyeti pamoja na kuwepo kwa mazingira rahisi ya kupata leseni ya Udereva.

Juhudi zote hizo za chuo cha WIDE INSTITUTE OF DRIVING ni kusaidia serikali katika juhudi za kutokomeza ajali za barabarani.

Ili kuhakikisha mafunzo hayo yanakuwa na matokeo chanya kwa wale wote wanaopatiwa wajitahidi kuzingatia ili kuleta tija na maendeleo katika sekta ya usafirishaji.

OKULY BLOG ipo hapa kwa ajili ya kukupatia kile kinachoendelea kuhusu mafunzo hayo yanayoendelea hapa BWALO LA POLISI MKOANI DODOMA.

No comments:

Post a Comment