Afisa Mlinda Mlaji kutoka FCC ,Thecla Kitosi,akitoa elimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia katika shule ya Msingi Bunge ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.
....
TUME ya Ushindani (FCC) leo Machi 19,2026 imetoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge kuhusu masuala ya kumlinda mlaji, ikiwemo haki na wajibu wa mlaji pamoja na madhara ya matumizi ya bidhaa bandia katika jamii.
Elimu hiyo imelenga kuwajengea wanafunzi uelewa wa awali kuhusu umuhimu wa kuchagua na kutumia bidhaa zilizo salama, huku ikisisitiza kuwa walaji wana nafasi kubwa katika kulinda afya zao na za wengine.
Mafunzo hayo pia yameenda sambamba na Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani, tukio linaloadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu haki za walaji duniani kote.
Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho hayo ni “Bidhaa Salama, Imani kwa Mlaji,” ikisisitiza umuhimu wa kuhakikisha bidhaa zote zinazotumiwa na wananchi zinakidhi viwango vya usalama na ubora.
Akizungumza na wanafunzi hao, Afisa Mlinda Mlaji kutoka FCC, Thecla Kitosi, amewahamasisha wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa elimu hiyo kwa jamii zinazowazunguka.
Aidha Bi.Kitosi amewaasa wanafunzi hao kuelewa haki zao kama walaji, pamoja na wajibu wao wa kutoa taarifa kwa FCC wanapobaini au kuwa na mashaka kuhusu usalama wa bidhaa au huduma wanazotumia.
Hata hivyo amewahimiza wanafunzi kuwa mabalozi wazuri kwa jamii zao kwa kuwafahamisha wazazi na ndugu zao juu ya hatari za bidhaa bandia na namna ya kuzitambua.
"FCC itaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii, hususan wanafunzi, ni njia muhimu ya kujenga taifa lenye walaji wenye uelewa, wanaoweza kujilinda dhidi ya bidhaa bandia na huduma zisizo na ubora."amesisitiza Bi.Kitosi
Kwa upande wake Mkaguzi wa Bidhaa bandia kutoka FCC Bi.Diana Augustine, amieleza kuwa bidhaa bandia zinaweza kuwa na athari kubwa kiafya, kiuchumi na hata kijamii. Alifafanua kuwa baadhi ya bidhaa hizo, hususan vipodozi, dawa na vifaa vya umeme, vinaweza kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji kutokana na kutokidhi viwango vya ubora vinavyotakiwa.
“Ni muhimu kwa kila mmoja wetu kuwa makini na bidhaa tunazonunua. Hakikisheni mnachunguza nembo za ubora na kununua bidhaa kutoka kwa wauzaji wanaoaminika,” amesisitiza Bi. Diana.
Kwa upande wao, wanafunzi walionesha shauku kubwa kwa kuuliza maswali mbalimbali kuhusu namna ya kutofautisha bidhaa halisi na bandia. Walishukuru kwa elimu hiyo na kuahidi kuitumia ipasavyo katika maisha yao ya kila siku.
Elimu hii ni sehemu ya juhudi za FCC za kuendelea kulinda haki za mlaji pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa salama na zenye ubora unaokubalika, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.

Afisa Mlinda Mlaji kutoka FCC ,Thecla Kitosi,akitoa elimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia katika shule ya Msingi Bunge ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.

Afisa Mlinda Mlaji kutoka FCC ,Thecla Kitosi,akitoa elimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia katika shule ya Msingi Bunge ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.

Afisa Mlinda Mlaji kutoka FCC ,Thecla Kitosi,akitoa elimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia katika shule ya Msingi Bunge ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.
Mkaguzi wa Bidhaa bandia kutoka FCC Bi.Diana Augustine akitoa elimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia katika shule ya Msingi Bunge ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.
Sehemu ya wanafunzi wakisikiliza mada mbalimbali wakati wakipata aelimu kuhusiana madhara ya bidhaa bandia katika shule ya Msingi Bunge iliyotolewa na FCC ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.

Wanafunzi wakiuliza maswali mbalimbali kuhusu namna ya kutofautisha bidhaa halisi na bandia mara baada ya kupatiwa elimu na FCC ikiwa ni sehemu ya kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Siku ya Haki za Mlaji Duniani.

Maafisa kutoka Tume ya Ushindani(FCC) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Bunge mara baada ya kukamilisha utoaji wa elimu kwa wanafunzi kuhusiana masuala ya kumlinda mlaji.

No comments:
Post a Comment