Kikosi bora Afrika hiki hapa, Sadio Mane hayumo - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 5, 2018

Kikosi bora Afrika hiki hapa, Sadio Mane hayumo


Usiki wa jana kulikuwa na tuzo za mchezaji bora wa Afrika zilizofanyika mjink Accra nchini Ghana, mchezaji wa timu ya taifa ya Misri ambaye pia anakipiga Liverpool Mohamed Salah alinyakua tuzo hiyo.

Kama kawaida katika ugawaji wa tuzo hiyo kunakuwa na kikosi bora cha Afrika, ambapo kwa mwaka 2017 katika kikosi hicho golikipa ni mlinda mlango wa timu ya taifa ya Tunisia Aymen Mothlouthi.

Walinzi katika kikosi hicho ni Ali Mooloul wa timu ya taifa ya Tunisia, Eric Bailly anaichezea Ivory Coast na pia Manchester United, Ahmed Fathy wa timu ya taifa ya Misri na Achraf Benchark wa Morocco.

Viungo ni Mohamed Ounaje wa timu ya taifa ya Morocco ambaye pia anakipiga Wydad Casablanca na Khalid Boutaib wa Tunisia huku washambuliaji wakiwa Mohamed Salah wa Misri, Juniour Ajayi wa Nigeria na Yassine Khenissi wa Tunisia.

Katika kikosi hiki maswali yamekuwa mengi haswa kutokana na kukosekana kwa majina makubwa kama Sadio Mane, Nabil Keita na Pierre Aubameyang ambao mwaka 2017 ulikuwa mwaka mzuri kwao.

No comments:

Post a Comment