Spika Ndugai ameyasema hayo katika maadhimisho ya wiki ya asasi za kiraia Azaki yanayofanyika Jijini Dodoma ambapo amesema ni wakati wa asasi hizo kijitathimini na kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria zinazowaongoza
Aidha amesema mbali na asasi za kiraia kutoa mchango mkubwa katika kujenga nchi lakini Endapo wataruhusu migogoro na migongano ndani ya asasi zao itakuwa ni jambo Gumu kwao kufanikisha malengo au hazma walizo jiwekea.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Wiki ya AZAKI aliyezungumza kwa niaba ya mashirika zaidi ya 20 Lulu Ng’wanakilala ametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu wa wiki hiyo huku akimshukuru Spika Ndugai kukubali kuwa mgeni rasmi.
“Tunakushukuru sana Spika kwani tumefarijika na uwepo wako kwa niaba ya serikali, Kamati ya maandalizi tunasema ahsante na maelekezo yako tumayepokea tu tutashiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo,”amesisitiza.
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Ludovic Otouh ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Wajibu amesema mchango wa AZAKI katika maendeleo ni mkubwa na wiki ya AZAKI yam waka 2019 imetoa faida kubwa ikiwemo kuongezeka kwa mijala , na mwaka huu washiriki wa AZAKI mwaka huu walikutana katika kikao cha siku mbili kuangalia mchango wa AZAKI, hivyo kwa kufuata sheria , kanuni na taratibu na kwamba mikakati yao ni kuendelea kuimarisha ushirikiano.
“Tutumie fursa hii mgeni kukuomba uruhusu wabunge wajumuike nasi katika mijadala itakayoendelea kwa juma zima hapa Dodoma , aidha tunawaribisha wananchi wa Dodoma ili wajionee kazi ambazo AZAKI zinafanya, na matarajio yangu katika wiki ya AZAKI ijayo ifanyike nje ya Dodoma ili wananchi wengine nao wanufaike,”amesema
Wiki ya asasi za kiraia inafanyika Jijini Dodoma ambapo asasi mbalimbali zinapata nafasi ya kukutana na kujadili mambo yahusuyo asasi hizo pamoja na kutoa Elimu mbalimbali kwa jamii.
No comments:
Post a Comment