NAFASI ZA AZAKI KATIKA KUSHIRIKI MAENDELEO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 28, 2021

NAFASI ZA AZAKI KATIKA KUSHIRIKI MAENDELEO



Mbunge wa Geita Mjini Constantine Kanyasu ameeleza nafasi za AZAKI katika kushiriki maendeleo na namna ambavyo vyombo mbalimbali vya serikali ikiwemo Bunge na Wizara vinavyoshiki katika kuhakikisha kero na changamoto za wananchi zinatatuliwa.

Ameyasema hayo katika mdahalo uliandaliwa na shirika la maendeleo ya mtoto(SAVE THE CHILDREN) ikiwa ni muendelezo wa midahalo inayoendelea katika Wiki ya AZAKI yanayofanyika jijini Dodoma.

Kanyasu ameelezea nafasi ya bunge katika kuleta ufanisi katika kutatua kero na changamoto za wananchi ikiwemo maswala ya bajeti, Kisheria na maoni mbalimbali ya kisera yanayotolewa na wanachi.

Ameongeza kuwa Bunge Lina kazi kubwa ya kujadili sera zilizopo kama bado zipo kwenye wakati ama zimepitwa na wakati na kuzibadilisha ili kuendana na kasi ya mabadiliko yaliyopo kwa sasa.



      
                           COSTANTINE KANYASU mbunge wa Geita mjini

Pia Kanyasu amezipongeza Azaki zote na kuwataka wananchi kuwa huku katika kutoa maoni na kushirikiana vyema na mashirika haya yasiyo ya kiserikali ili kuhakikisha maendeleo yanayopatikana yanakuwa jumuishi bila kuacha yeyote.

Kwa upande wake Meneja Utetezi na Uchechemuzi wa shirika la Maendeleo ya mtoto (Save theChildren) Ndugu Oscar Mrema ametoa historia fupi ya kuanzishwa kwa shirika hili pamoja na vipaumbele vyao katika kuhakikisha kuwa mtoto anapata makuzi mazuri tangu kuzaliwa pamoja na kupata haki ya kupata elimu Bora pamoja na mahitaji mengine ya msingi.

Amesema shirika la maendeleo ya watoto limeanzishwa rasmi hapa nchini mwaka 1986 kwa lengo la kusimamaa haki na maendeleo yamtoto pamoja na Ulinzi wa mtoto.

Pamoja na hayo ameongeza kuwa wanamiradi mbalimbali ikiwemo ya Afya na kuhamasisha ulinzi wa mtoto na kuhakikisha hilo Shairika la Maendeleo ya mtoto linakikisha kunakuwepo na mabaraza ya watoto ili kuwapa fursa ya kuweza kufanya maamuzi kwenye jamii.

Pia amesema kuwa wanahakikisha pia mtoto anapata lishe bora na wanashirikiana na serikali ili kuhakikisha watoto wanapata lishe bora hata kabla ya kuzaliwa ili kujengea afya ya kuyosha ya akili na uwezo mzuri wa kufanya maamuzi.

Akizungumza kwa niaba ya vyombo vya habari na wadau wake ndugu SULEIMANI ABEID ambae ni mgeni mualikwa kutoka Mkoani Shinyanga amesema kuwa SAVE THE CHILDREN imesaidia sana wananchi kufumbua macho katika maswala mbalimbali ikiwemo bajeti.

Pia amegusia nafasi ya vyombo vya habari katika kuleta maendelea kwa taifa kwa kushirikiana vyema na Azaki ambapo ametoa rai kwa wanahabari kutokuwa na wasiwasi katika kuripoti matukio yanayotokea katika jamii ili kufanya jamii iwe salama

Naye kiongozi wa Haki za mtoto katika shirika la Maendeleo ya mtoto (Save the Children) bwana Wilbert Muchukuzi amesema kuwa jamii inawiwa kuhakikisha zile haki za msingi ya mtoto Inalindwa ili kumsaidia katika kuondokana na ukatili ambao umekuwa unakithiri kila kukicha katika jamii zetu za

Wiki ya Azaki 2021 imekuwa ikiibua hoja nyingi za msingi ambazo zimekuwa zikitolewa na watu mbalimbali kutoka kada mbalimbali wakiwemo Mawaziri na wabunge pamoja na wageni wengine toka sekta za serikali na sekta binafsi hoja hizo zikiwa na lengo la kuikosoa na kuionesha njia sahihi serikali katika kutekeleza majukumu yake bila kuvunja haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment