Maelfu wakusanyika katika miji ya Australia kupinga chanjo ya Covid-19 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 20, 2021

Maelfu wakusanyika katika miji ya Australia kupinga chanjo ya Covid-19



Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika katika miji kadhaa ya Australia leo Jumamosi, kupinga chanjo dhidi ya Covid-19. Mpango wa chanjo ya corona nchini humo bado umebaki kuwa hiari na wenye mafanikio makubwa ambapo karibu asilimia 85 ya idadi ya watu kuanzia umri wa miaka 16 wamepatiwa chanjo kamili.


Lakini waandamanji wamekusanyika Jumamosi katika miji kadhaa mikubwa nchini Australia dhidi ya mamlaka ya chanjo. Polisi wanasema kiasi ya waandamanaji 10,000 wamekusanyika mjini Sydney.


Waandamanaji wengine wapatao 2,000 wamefanya maandamano mjini Melbourne lakini ya kupinga maandamano yanayopinga chanjo. Australia imerekodi visa 195,000 na vifo 1,933 vya corona katika idadi jumla ya watu zaidi ya milioni 25 tangu kuanza kwa mlipuko wa corona


No comments:

Post a Comment