Ethiopia yaonya mashirika ya habari kutokana na vita ya Tigray - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, November 20, 2021

Ethiopia yaonya mashirika ya habari kutokana na vita ya Tigray



Mamlaka ya vyombo vya habari nchini Ethiopia imeyaonya mashirika manne ya kimataifa ya habari na kutishia kufuta leseni yake kwasababu ya kuripoti kuenea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika mkoa wa Tigray. 


Mashirika yaliyopewa onyo ni pamoja na BBC, CNN, Reuters na AP. Katika taarifa yake, serikali imesema kuwa imekuwa ikifuatilia mwenendo wa ripoti za mashirika hayo juu ya operesheini ya utekelezaji wa sheria katika mkoa wa kaskazini, na kwamba mashirika yaliyotajwa yamekuwa yakieneza habari kila mara ambazo zinachochea uadui. 


Nalo shirika la usalama wa mtandao wa mawasiliano wa Ethiopia, umeziamuru balozi, wanadiplomasia na watu binafsi kusajili baadhi ya vifaa vya kielekroniki kama vile redio za kutuma na kupokea mawasiliano na simu za sateraiti ili visiweze kutumiwa na magaidi


No comments:

Post a Comment