Matamshi hayo yametolewa na waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin katika mkutano wa mjini Manama, Bahran. Austin ameongeza njia zote ziko wazi ikiwa diplomasia itashindwa katika kuzuia mipango ya nyuklia ya Iran.
Waziri huyo hata hivyo amelazimika kukanusha madai ya kwamba Marekani imekuwa ikisita kutumia nguvu na kwamba itaendelea kujilinda na kutetea maslahi yake. Iran inatarajia kurejea tena katika meza ya mazungumzo na mataifa yaliyo na nguvu duniani, katika mazungumzo yatakayofanyika Novemba 29.
Mazungumzo hayo yanalengo la kufufua mkataba wa nyuklia wa 2015 na uwezekano wa kuondolewa vikwazo iliyowekewa Iran
No comments:
Post a Comment