Kabla ya tukio hilo marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na alitelekezwa na mke wake hali iliyopelekea kukata tamaa ya maisha na siku chache zilizopita alifanya jaribio la kujilipua kwa Petrol kabla ya kuokolewa na mdogo wake.
"Mnamo tarehe 08.11.2021 majira ya saa 03:00 asubuhi huko Kijiji cha Ihombe kilichopo Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, na mtu mmoja amekutwa ameungua na moto nyumbani kweke Upelelezi wa shauri hili unaendelea" Kamanda wa polisi Mbeya.
Aidha ninatoa wito kwa wananchi/jamii kwa ujumla kutoa taarifa za mtu/watu wenye hali ya kukata tamaa ya Maisha kwa viongozi wao wa vijiji, mitaa kabla ya kutokea madhara makubwa kama ilivyotokea kwa marehemu MASHAKA SAIMON @ YOKONIA.
No comments:
Post a Comment