![]() |
Mgeni rasmi Fidelis Kaishozi (katikati)Ambaye ni Afisa Rasirimali kutoka kiwanda Cha kuzalisha wine ya Alco Vintages |
VIJANA kote nchini wametakiwa kujiepusha na vitendo vya anasa na starehe ambavyo vinaweza kuwasababishia kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo UKIMWI licha ya Wengi kuuchukulia kitu Cha kawaida .
Hayo yalielezwa na Fidelis Kaishozi Ambaye ni Afisa Rasirimali kutoka kiwanda Cha kuzalisha wine Alco Vintages ,wakati alipokuwa mgeni Rasmi kwenye mahafali ya kidato Cha nne Taasisi ya watu wazima Mkoa wa Dodoma.
Aidha Kaishozi alisema kuwa Vijana wanapomaliza masomo yao ni muda muafaka kwao kijiunga na vyuo mbalimbali vya vyeta ambavyo vitawasaidia kuwa na ujuzi utakaowasaidia kwenye maisha yao ,na sio kutumia muda huo kujiingiza kwenye makundi hatarishi .
Alisema kuwa Vijana Wengi wamekuwa na dhana potofu kwamba wanapomaliza masomo ni fursa kwao kwenda kwenye starehe na Tabia mbaya ikiwemo ulevi,uasherati,wizi na wengine kuendekeza ngono bila kujali ugonjwa wa UKIMWI kwa madai kwamba ni ajali na kitu Cha kawaida jambo ambalo sio kweli.
"Niwasihi msiridhike na elimu hiyo bali iwe Chachu kijiendeleza kupata elimu sehemu pia niwaombe mjiepushe na vikundi vya mitaani hasa madawa ya kulevya ulevi,umalaya na mambo mengine kwa Sasa Kuna janga la Taifa utakuta Vijana sokoni wanatumia vilevi kuliko hata konyagi na ukiwaona wanayumbayumba na matokeo yake hawawezi kufanikiwa kwenye maisha yao"alisema Kaishozi
Alitumia nafasi hiyo Kutoa wito kwa jamii nzima kutekeleza Agizo la Serikali la kuchanja chanjo ya Corona 19 ambao ugonjwa huo unaua haraka kuliko hata ukimwi.
Nae Mkurugenzi Taasisi ya elimu ya watu wazima Daktari Michael Ng'umbi alisema aliwataka Wazazi kuwekeza elimu kwa watoto na kuwalipa mahitaji muhimu ikiwemo karo kwani elimu ndiyo utajiri wa kudumu kuliko nyumba ,magari ,mashamba ambavyo vinaweza kuuzwa muda wowote na kutapanya fedha.
"Niwaahidi ambaye atakaye faulu kwenda kidato Cha tano nitampa laki tatu kwa ajili ya madaftari na matumizi madogo hivyo kwa hiyo ni jitihada zenu kuhakikisha mnafanya vizuri,
Alisema kutokana na uwepo wa makao Makuu hapa Jijini Dodoma Taasisi kupitia Serikali kwa bajeti ya mwaka huu wataweka hadhi ya Taasisi ili iendane na makao Makuu ambapo watajenga uzio , vyoo na ukarabati wa jengo na kwamba wakati mwingine waweze kufanyia vikao vyao hapa na sio Jijini Dar es salaam.
Awali akisoma Risala Mkufunzi Mkazi Mkoa wa Dodoma Anna Ntiruvakule alisema ni mahafali ya kwanza tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo ambapo wahitimu 88 licha ya mafanikio na changamoto zilizopo.
"Tumefanikiwa Kutoa fursa kwa watu kujiendeleza kielimu kwa gharama nafuu , Kutoa ajira za muda kwa walimu wanaofundisha kwenye vituo vyetu,kuchaguliwa kwa wanafunzi kijiunga kidato Cha tano shule za Serikali na vyuo "
"Licha ya hayo tuna changamoto ya uhaba wa vyumba vya Madarasa na Ofisi kwa ajili ya walimu na wakufunzi,vifaa vya kujifunza na kujifunza na zipo changamoto za ulipaji ada Kwa wakati toka kwa Wazazi walezi na wanafunzi wanaojilipia wenyewe"alisema Anna.
Kwa upande wao wahitimu walisema kuwa elimu waliyoipata wataenda kuwa Vijana Bora kwenye Jamii huku wakiuomba Uongozi wa chuo kuendelea kuboresha miundo mbinu ambayo atawasaidia Katika ujifunzaji mzuri.
No comments:
Post a Comment