Na Okuly Julius, Dodoma
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DKT.STERGOMENA LAWRENCE TAX AKIZUNGUMZA KATIKA WARSHA HIYO |
HAYO YAMESEMWA JIJINI DODOMA NA WAJUMBE WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA NA ILE YA BARAZA LA WAWAKILISHI YA VIWANDA NA BIASHARA YA ZANZIBAR WAKATI WAKIPOKEA MAWASILISHO YA MKATABA HUO KUTOKA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA.
KATIKA WARSHA HIYO AMBAE IMEHUDHURIWA PIA NA WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA DKT.STERGOMENA LAWRENCE TAX AKIMUWAKILISHA WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AMESEMA KUWA TANZANIA IMEJIANDAA KIKAMILIFU KATIKA KUTEKELEZA MKATABA HUO AMBAO KWA KIASI KIKUBWA UTACHANGIA KUKUA KWA UCHUMI HAPA NCHINI.
KWA UPANDE WAKE MKURUGENZI WA IDARA YA MTANGAMANO WA BIASHARA ALLY GUGU AMBAE NDIYE AMEWASILISHA MAELEZO JUU YA MKATABA HUO MBELE YA WANAKAMATI NA WASHIRIKI WA WARSHA HIYO AMESEMA LICHA YA MKATABA HUO LAKINI NCHI ITAKUWA HURU KUAMUA MAMBO YAKE IKIWAMO KULINDA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NDANI.
Ameongeza kuwa Mkataba wa AfCFTA umezingatia maslahi mapana ya nchi wanachama kama Kuvilinda viwanda vichanga,Usalama wa chakula,Upotevu wa mapato ya serikali,Sekta zinazozalisha ajira kwa watu wengi,Sekta za kimkakati na Uhuru wa kisera mambo ambayo yatafanya kila mwanachama kuwa mnufaika katika mkataba huu.
Pamoja na hayo ameongezea faida mbalimbali zitapatikana kwa nchi ambazo zitaridhia mkataba huu kuwa ni pamoja na kuingiza biashara zao katika nchi wanachama bila kutozwa kodi kubwa ya ushuru katika bidhaa zinazozalishwa ndani ya bara la Afrika kwa 97% Ndani ya miaka kumi ijayo ikiwa ni makubaliano ya wakuu wa nchi za Bara la Afrika.
Pia ameziomba serikali hizi mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar kuondoa vikwazo vilivyopo vya kibiashara ili kuruhusu wanachi kufanya biashara kwa uhuru na usawa ili kuchochea maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment