JIJI LA DODOMA LAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS DKT.PHILIP MPANGO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 17, 2022

JIJI LA DODOMA LAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS DKT.PHILIP MPANGO


Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru akizungumza na Watendaji wa kata na hii ni baada ya agizo la Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango la kutaka jiji la Dodoma kuwa safi ndani ya wiki mbili.


Na Okuly Julius, Dodoma 

Agizo la Makamu wa Rais Dkt. Mpango la kulitaka jiji la Dodoma kuwa safi ndani ya wiki mbili laanza kutekelezwa

Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Dodoma wameanza kutekeleza agizo la makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango alilolitoa juzi la kuwataka hakikisha jiji hilo ambalo ni makao makuu ya nchi linakuwa safi na kusitiza mkataba na Kampuni ya usafi wa mazingira ya Green West iliyokuwa ikihudumu katika jiji hilo.

Hayo yalijili jijini Dodoma wakati wa kikao baina ya uongozi wa mkoa na watendaji wa kata kutoka maeneo yote ya jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mafuru amewataka Watendaji, maafisa afya na Mazingira kufuaata sheria za mazingira kwa kutoa Faini kama kuna mtu anastahili adhabu hiyo.

" Kuanzia sasa mimi na timu yangu tutanza kutembea mtaa kwa mtaa kata kwa kata ili kuona kama zoezi hili linafanyika ipasavyo kwani ni ukweli kwamba watu wako makao makuu lakini hawafanyi kazi ka kujituma ipasavyo wakati kuna watumishi wengine wako huko pembezoni wanatamani kuja makao makuu," amesema

Amemuagiza Afisa Utumishi kuorodhesha majina ya watumishi ambao hawakuweza kufika katika kikao hicho ili kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru kutowaonea huruma watumishi wote walio chini yake wakiwemo wakuu wa Idara na watendaji wa kata pale anapoona wanashindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuwabadilishia vituo vya kazi wale waliopo chini ya Mamlaka yake.

Pia amesisitiza kuwa uongozi wa jiji hilo kuhakikisha suala la kuzagaa kwa taka linakuwa historia huku akiweka mikakati kabambe ya kumaliza changamoto hiyo.

Aidha Mtaka amemuagiza Mkurugenzi huyo kuwabadilisha vituo vya kazi watendaji wa Kata na Mitaa ambao utendaji kazi wao umekuwa sio mzuri huku akisisitiza kutoa kipaumbele kwa wale ambao ni watendaji wabunifu.

Hata hivyo kikao hicho cha mikakati ya utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais, Dkt Mpango kimekuja baada kuwataka viongozi wa jiji la Dodoma kuhakikisha ndani ya wiki mbili Dodoma ionekane safi katika Kata na Mitaa yote.

Pia ametoa maelekezo ya kutoonekana kwa kibada chochote cha machinga katikati ya Mji wala Mitaani kwani machinga wote wameshasajiliwa na kujengewa soko ambapo ameeleza kuwa kwa kufanya hivyo itasidia kuepusha migogoro kati ya machinga na Serikali.

Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Dodoma Dkt.Fatma Mganga amewataka Maafisa Mazingira na Maafisa Afya bila kuwasahau Watendaji wote kuwaonyesha wananchi kufanya usafi kwa vitendo na mifano ili iwe njia mojawapo ya kuwaonesha wananchi na wao wahamasike kufanya usafi .

" hapa nimesikia kunajumla ya watendaji 239 walioajiriwa serikalini sasa kunasababu gani ya jiji lionekane chafu...hapa kunamahali hatuwajibiki ipasavyo na iko wazi tumejisahau sehemu hivyo lazima tujiulize ni kwanini tumefika hapa mpaka viongozi wa juu wanakuja kutukosoa kwamba sisi Mkoa wa Dodoma wachafu ," amesema Katibu Tawala huyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabiri Shekimweri amesema mkakati wa usafi wa Mazingira katika jiji la Dodoma liwe la muendelezo ili tuwape imani viongozi wetu wa juu.

Mbali na hayo Shekimweri amependekeza kuajiriwa kwa watu maalumu watakaokuwa na kazi ya kuzunguka maeneo yote ya jiji la Dodoma kukagua mpangilio na maendeleo ya usafi katika kila kona na wapewe Makali ya kutosha ili wakibaini kukiukwa kwa utaratibu wawe na uwezo wa kupiga faini ikiwezekana kuwakamata pia waliokiuka utaratibu.


No comments:

Post a Comment