Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Yusufu Masauni ameyasema hayo Leo katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma katika kikao na Uongozi wa juu wa Jeshi la Polisi kujadili kadhia ya mauaji yanayoendelea nchini ili kupata ufumbuzi wakudumu kwakujiridhisha na kufanya tathmini ili kujua nini kifanyike ambapo amepokea taarifa ya Mwezi mmoja kuhusiana na matukio hayo.
Pamoja na hayo Waziri Masauni ameunda Kamati ya kuishauri Serikali nini kifanyike ili kupata suluhisho lakudumu la matatizo hayo ambapo ndani ya siku 21 ije na Mkakati wa Kitaifa kuhakikisha wanadhibiti changamoto hiyo.
Katika kamati hiyo kutakuwa na wawakilishi kutoka Wazara ya Mambo ya Ndani,Jeshi la Polisi,Usalama wa Taifa,TAKUKURU, Elimu ya Vyuo Vikuu,Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya DPP na Wazara ya Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kuhusiana na matukio hayo kwani masuala hayo sio la Jeshi la Polisi pekee kwani Wadau wengine wanahitaji kushiriki,zaidi ya matukio 30 ni ya kugombania Mali,Mirathi,wivu wa mapenzi,visasi,ushirikina,migogoro ya Ardhi,ulevi pamoja na kujichukulia Sheria mkononi.
Katika hatua nyingine Waziri Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha wahusika wa mauaji ambao hawajakamatwa katika maeneo mengine wanakamatwa mara Moja huku akiwa na imani kuwa jeshi la polisi Lina uwezo mkubwa kupitia vyombo vyake.
No comments:
Post a Comment