Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP James Manyama, na kusema tukio hilo limetokea jana Januari 4, 2022, na kwamba waliopoteza maisha ni watoto wanne kutoka familia tofauti na mwingine akipigwa na radi na kupoteza maisha wakati akiwa anaendelea kulima shambani.
Aidha, Kamanda Manyama ametoa tahadhari kwa wananchi mkoani Kigoma hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mvua ili kuepusha madhara zaidi.
Chanzo - EATV
No comments:
Post a Comment