BAADA YA SADC KUITAJA TANZANIA KINARA WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA; KAMISHNA LUOGA ATAKA WATUMISHI KUKUZA MATUMIZI YA NISHATI HIYO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 18, 2026

BAADA YA SADC KUITAJA TANZANIA KINARA WA NISHATI SAFI YA KUPIKIA; KAMISHNA LUOGA ATAKA WATUMISHI KUKUZA MATUMIZI YA NISHATI HIYO


Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga
akifungua kikao cha Tatu cha Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi
la Wizara ya Nishati kwa niaba ya Ma-Katibu Wakuu wa Wizara ya
Nishati. Mkutano huo umefanyika tarehe 18 Machi 2026 jijini Dodoma

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Nishati wakiwa katika
Mkutano wa Pili wa Baraza hilo uliofanyika jijini Dodoma tarehe 18
Machi 2026 jijini Dodoma


Na Mwandishi Wetu 


Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga
amewataka Watumishi wa Wizara ya Nishati kuendelea kukuza matumizi ya
nishati safi ya kupikia nchini ili kufanikisha ajenda hiyo ambayo
kinara wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia
Suluhu Hassan.

Ameeleza kuwa ajenda ya nishati safi ya kupikia tayari imeanza
kuonesha mafanikio nchini na hivyo kupelekea Tanzania kutambuliwa
katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo katika nchi zilizo katika
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Kamishna Luoga amesema hayo tarehe 18 Machi 2026 jijini Dodoma wakati
akifungua kikao cha Tatu cha Mkutano wa Pili wa Baraza la Wafanyakazi
la Wizara ya Nishati kwa niaba ya Ma-Katibu Wakuu wa Wizara ya
Nishati.

“Katika Mkutano wa SADC ambao Tanzania ilishiriki hivi karibuni,
kupitia hotuba mbalimbali zilizotolewa katika mkutano huo ikiwemo ya
mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa
aliitambua na kuipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kwenye matumizi ya
nishati safi ya kupikia, lakini pia katika maazimio ya mwisho
yaliyoandaliwa na sekretarieti ya SADC, nchi zote za SADC zilitakiwa
kuunga mkono juhudi hizo za Tanzania.” Amesema Kamishna Luoga

Kutokana na hilo, amempongeza Rais, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
juhudi anazochukua kufanikisha ajenda ya nishati safi ya kupikia, pia
amewapongeza Watumishi Wizara ya Nishati kwa kufanikisha juhudi hizo
ambazo zinalenga kuimarisha afya za watanzania na kupunguza uharibifu
wa mazingira.

Aidha, katika kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi kilicholenga
kujadili, kutoa maoni, ushauri na kupitisha mapendekezo ya Bajeti ya
Wizara ya Nishati kwa mwaka 2026/2027, Mhandisi Luoga amewataka
wajumbe wa Baraza kujiridhisha kuhusu maeneo yote muhimu ya vipaumbele
vya Wizara kama yametengewa fedha ili kuwezesha Wizara kuhudumia
watanzania kwa ufanisi.

Vilevile, amewataka Watumishi kuzingatia maadili ya utumishi wa umma
katika utekelezaji wa majukumu yao na kujiepusha na utoro, rushwa na
kutanguliza uzalendo katika kuwahudumia watanzania.

Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Nishati umehudhuriwa pia na
Viongozi wa TUGHE Mkoa na Tawi la Nishati, pamoja wawakilishi kutoka
Taasisi zilizo chini ya Wizara

No comments:

Post a Comment