WIZARA YA FEDHA YAENDELEA NA UCHAMBUZI WA BAJETI SEKTA YA UZALISHAJI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 18, 2026

WIZARA YA FEDHA YAENDELEA NA UCHAMBUZI WA BAJETI SEKTA YA UZALISHAJI


Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, Bw. Fundi Makama, akiongoza kikao kazi cha wataalamu wa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa cha kupitia, kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti yaliyowasilishwa na Sekta ya Uzalishaji ikiwemo, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Madini ili kuhakikisha kuwa yanazingatia vipaumbele na Mipango ya Taifa, sera na mikakati ya maendeleo, pamoja na miongozo ya upangaji na uandaaji wa bajeti, kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, (Treasury Square) jijini Dodoma.

Mkurugenzi kutoka, Idara ya Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini, Tume ya Taifa ya Umawagiliaji, Dkt. Consolatha Kapinga, akiwasilisha vipaumbele vya Tume hiyo wakati wa Kikao Kazi cha wataalam wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa cha kupitia, kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti yaliyowasilishwa na Sekta ya Elimu ili kuhakikisha kuwa yanazingatia vipaumbele na Mipango ya Taifa, sera na mikakati ya maendeleo, pamoja na miongozo ya upangaji na uandaaji wa bajeti, kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, (Treasury Square) jijini Dodoma.

Wataalam wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, wakifuatilia Kikao kazi cha kupitia, kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti yaliyowasilishwa na Sekta ya Uzalishaji ikiwemo, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Madini ili kuhakikisha kuwa yanazingatia vipaumbele na Mipango ya Taifa, sera na mikakati ya maendeleo, pamoja na miongozo ya upangaji na uandaaji wa bajeti, kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, (Treasury Square) jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mipango na Bajeti, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Godfrey Machabe, akiwasilisha vipaumbele vya wizara hiyo wakati wa Kikao Kazi cha wataalam wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa cha kupitia, kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti yaliyowasilishwa na Sekta Elimu ili kuhakikisha kuwa yanazingatia vipaumbele na Mipango ya Taifa, sera na mikakati ya maendeleo, pamoja na miongozo ya upangaji na uandaaji wa bajeti, kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, (Treasury Square) jijini Dodoma.

Kikao kazi cha wataalam wa Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa cha kupitia, kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti yaliyowasilishwa na Sekta Elimu ili kuhakikisha kuwa yanazingatia vipaumbele na Mipango ya Taifa, sera na mikakati ya maendeleo, pamoja na miongozo ya upangaji na uandaaji wa bajeti, kikiendelea katika Ukumbi wa Kambarage, Wizara ya Fedha, (Treasury Square) jijini Dodoma.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF - Dodoma)


Na. Jordan Mbwambo, WF - Dodoma


Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, inaendelea na uchambuzi wa bajeti ya sekta ya uzalishaji kwa mwaka wa fedha 2026/2027. Sekta hiyo inajumuisha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Madini.

Hatua hiyo inalenga kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti ya sekta muhimu za uzalishaji ili kuhakikisha yanazingatia vipaumbele vya Taifa, sera za maendeleo, mikakati ya kitaifa pamoja na miongozo ya upangaji na uandaaji wa bajeti.

Kikao hicho kimeongozwa na Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, Bw. Fundi Makama na kuhudhuriwa na Wakurugenzi wa Sera na Mipango pamoja na wataalamu kutoka wizara na sekta husika.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Kambarage, Treasury Square, jijini Dodoma ambapo, washiriki walipata nafasi ya kujadili kwa kina namna bajeti za sekta za uzalishaji zinavyoweza kuyafikia malengo yaliyowekwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na kuimarisha uchumi wa Taifa na kuchochea maendeleo endelevu.

No comments:

Post a Comment