PROF. NOMBO, e-GA WAWEKA MKAKATI KUIMARISHA MIFUMO YA TEHAMA SEKTA YA ELIMU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 25, 2026

PROF. NOMBO, e-GA WAWEKA MKAKATI KUIMARISHA MIFUMO YA TEHAMA SEKTA YA ELIMU


​Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imejipanga kuimarisha na kuongeza ufanisi wa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) inayotumika katika sekta ya elimu nchini, ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya kidijitali.

Hatua hiyo inafuatia kikao cha pamoja kilichofanyika leo Mei 25, 2026, jijini Dodoma kati ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA), Mhandisi Benedict Ndomba, kwa lengo la kutathmini na kuboresha mifumo hiyo.

Mbali na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na utoaji huduma, mazungumzo hayo yamegusia kwa kina umuhimu wa kuongeza ulinzi na usalama wa mifumo na kanzidata (databases) za sekta ya elimu ili kuzuia vihatarishi vya kimtandao na kulinda taarifa muhimu za serikali na wadau wa elimu.

Ushirikiano huo kati ya Wizara ya Elimu na e-GA unatarajiwa kuleta mapinduzi katika usimamizi wa mifumo ya TEHAMA, huku ukihakikisha kuwa mifumo yote inayotumika inasomana na kubadilishana taarifa kwa urahisi na usalama wa hali ya juu.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Prof. Daniel Mushi, Wataalam wa masuala ya TEHAMA kutoka Wizara ya Elimu na wale wa e-GA






No comments:

Post a Comment