TANZANIA YAZINDUA MKAKATI WA KITAIFA WA ELIMU JUMUISHI WA MIAKA MITANO [2021/22-2025/26 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 29, 2022

TANZANIA YAZINDUA MKAKATI WA KITAIFA WA ELIMU JUMUISHI WA MIAKA MITANO [2021/22-2025/26



Serikali ya Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imezindua mkakati wa Kitaifa  wa Elimu jumuishi wa miaka mitano [2021/22-2025/26] uliofanyika jijini Dodoma

Na,Okuly Julius, Dodoma 
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa miaka mitano 2021/2022 hadi 2025/ 2026 wenye lengo la kutoa elimu hiyo kwa makundi yote maalumu.

Akizungumza katika uzinduzi wa mkakati huo Januari 28,2022 jijini Dodoma Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Eliamani Sedoyeka  amesema mpango wa serikali ni kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu bora bila kujali hali aliyo nayo.

Aidha,amesema elimu jumuishi ya awamu iliyopita ilizingatia elimu Msingi na elimu ya Sekondari na mkakati Jumuishi wa awamu hii umezingatia katika ngazi zote za elimu.

Hata hivyo,amesema mpango huo ni katika kuhakikisha wanafunzi wanajengewa uwezo na kuimarisha ukusanyaji wa taarifa .

Ametoa wito kwa wadau wote wa elimu Tanzania kuwa wanafikisha taarifa sahihi umuhimu wa elimu Jumuishi ili kila mtu anakuwa na haki ya kupata elimu ikiwemo makundi ya watu wenye mahitaji maalum.


Katibu Mkuu wa Wizara wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa na wadau pamoja na wanafunzi wakionyesha vitabu vya muongozo mara baada ya kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika jijini Dodoma.


Kamishna wa Elimu Tanzania  Dkt.Lyabwene Mtahabwa    amesema kila mtu ana haki ya kupata elimu bora na kumnyima mtu elimu bora ni kumwandaa kuwa mtumwa katika karne hii ya 21.

Hivyo,kupitia Umakini wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuweka kipaumbele upatikanaji wa elimu kwa makundi yote ni vyema kila   mmoja  kuunga jitihada za utoaji elimu bora.

Mkurugenzi wa Elimu Maalum kutoka Wizara ya Elimu Magreth Matonya amesema katika mkakati huo itakuwa inafanyika tathmini kila baada ya miezi 6. 

Kwa upande wake katibu wa chama cha Mapindizi (CCM), Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga amesema Wizara hiyo imefanya jambo jema kuanzisha elimu jumuishi kwa watoto wote kwa kuona nao wanauwezo kupata elimu hiyo kama watoto wengine.

"Kama CCM tutaenda kuhamasisha wazazi wa wenye watoto wa makundi maalumu na mwaka huu tunachaguzi za ndani ya chama hivyo tutahamasishana," amesema.

Kamishina wa Elimu Tanzania Dkt.Lyabwene Mtahabwa,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika jijini Dodoma.



Mwakilishi Mkazi wa Mashirika ya Kimataifa Dkt.Daniel Baheta,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika jijini Dodoma.


Mkurugenzi wa Elimu Maalum na Jumuishi kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknlojia Dkt.Magreth Matonya,akielezea lengo la mkakati huo wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika jijini Dodoma.


Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma Pili Mbaga,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Elimu Jumuishi wa mwaka 2021/22-2025/26 uliofanyika jijini Dodoma.




No comments:

Post a Comment