TISA (9) WAJITOSA KUMRITHI NDUGAI KITI CHA SPIKA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 31, 2022

TISA (9) WAJITOSA KUMRITHI NDUGAI KITI CHA SPIKA.


Na, Okuly Julius, Dodoma 
Zoezi la uteuzi na utaratibu wa uchaguzi wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limekamilika leo jijini Dodoma.

Akizungumzia kukamilika kwa zoezi hilo Katibu wa Bunge na Msimamizi wa Uchaguzi huo Bi.Nenelwa J. Mwihambi amesema kuwa hadi kufikia saa 10:00 jioni ya tarehe 31/01/2022 ambapo ndio mwisho wa kuwasilisha majina ni wagombea (9) pekee ndio majina yao yamewasilishwa na kukidhi matakwa ya kisheria.

Miongoni mwa wagombea hao nane (8) sio Wabunge huku mgombea mmoja ndio Mbunge.

Katika hatua nyingine ameongeza kuwa wagombea hawa wapo wanawake (2) na wanaume (7) ,ambapo kesho tarehe 1 Februari , 2022 majina yao yatawasilishwa mbele ya wapiga kura ambao ni Waheshimiwa Wabunge.

Ameyataja majina hayo kuwa ni Bwn.Abdullah Mohammed Said (NRA),Eng.Aivan Jackson Maganza (TLP),Bwn.David Daud Mwaijojele (CCK),Bwn.Georges Gabriel Bussungu (ADA - TADEA),Bwn.Kunje Ngombale Mwiru (SAU).

Pamoja na hao wengine ni Bi.Maimuna Said Kassim (ADC),Bwn.Ndonge Said Ndonge ( AAFP),Bwn.Saidoun Abrahamani Khatibu (DP) na aliyekuwa Naibu Spika wa Bunge hilo Mhe.Dkt.Tulia Ackson kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nenelwa J. Mwihambi amemaliza kwa kuvishukuru vyama vyote vya siasa vilivyojitokeza pamoja na wagombea wao kwa ushirkiano walioipa ofisi yake hadi kukamilika kwa zoezi la uteuzi.

No comments:

Post a Comment