NAPE:SHERIA,KANUNI NA SERA ZOTE ZILIZOPITWA NA WAKATA KUPITIWA UPYA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, January 26, 2022

NAPE:SHERIA,KANUNI NA SERA ZOTE ZILIZOPITWA NA WAKATA KUPITIWA UPYA



Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye amesema serikali itapitia sharia,kanuni na sera zote zilizopitwa na wakati ili kurahisisha utekelezaji wa majukukumu ndani ya Wizara.

Nape amebainisha hayo leo Januari 26,2022 jijini Dodoma wakati akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa 28 Baraza kuu la wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania unaokwenda sambamba na mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa baraza hilo.

Waziri Nape amesema Wizara yake itahakikisha inasimamia haki za watu kwa maslahi mapana ya Taifa na kupitia sheria kanuni na sera zilizopitwa na wakati ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya kiutendaji.

Kuhusu Mafunzo hayo Waziri Nape amesema yatasaidia kuwajengea uwezo watumishi na kuifanya Tanzania ya kidijitali.


Pia ametumia fursa hiyo kulipongeza Shirika la Posta Tanzania kwa jitihada inayoendelea kufanya huku akisema serikali itaendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Sambamba na hilo Mheshimiwa Nape amewataka wafanyakazi Shirika la Posta Tanzania kuambizana ukweli katika utekelezaji wa majukumu kwani ukweli una gharama.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Jim Yonazi amesema Shirika la Posta Tanzania limefanya mabadiliko ya kiuchumi hivyo Wizara itaendelea kulisaidia ili kuendelea kuimarika Zaidi katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Kwa upande wake Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Mbodo amesema Shirika hilo limekuwa na mchango mkubwa kuhudumia jamii katika masuala ya usafirishaji mizigo na mawasiliano.



No comments:

Post a Comment