Na,Okuly Julius, Dodoma
Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru amesema swala la usafi kwa sasa limeimarika na hili ni kutokana na kuingia mikataba na kampuni nne za kufanya usafi katika kata nane za jiji hilo.
Ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo mbalimbali ya miradi ambayo inaendelea kutekelezwa chini ya uongozi wake.
Pamoja na hayo Mafuru amasema kuwa Makampuni manne amboa wameingia nao mkataba wa mwaka mmoja kuna kipengele wameweka katika mkataba ambapo ikionekana kuwa usafi hauridhishi basi moja kwa moja mkataba unakuwa umevunjika.
"Tumeingia mkataba wa mwaka mmoja na makampuni manne lakini ndani ya mkataba huo kuna kipengele cha kuvunja mkataba kama hatutaridhika na usafi wanaofanya" Amesema Mafuru
Hivyo kayataka makampuni hayo kuhakikisha wanafikia malengo ya kulifanya jiji la Dodoma kuwa eneo la kuvutia kwa usafi na mazingira kwa ujumla.
Ameongeza kuwa wananchi pia wamehamasika kufanya usafi katika maeneo yao huku akibainisha kuwa kila jumamosi wamekuwa wanapita Kata moja moja ili kuendelea kutoa elimu na hamasa kwa wananchi juu ya usafi wa Mazingira na kushiriki kwa vitendo katika kufanya usafi.
Aidha,Mafuru ameeleza kuwa mpaka sasa Halmashauri ya jiji la Dodoma imekwisha panda miti milioni tatu katika maeneo mbalimbali ikiwemo kandokando ya barabara ,mashuleni na maeneo mengine huku kila mwanafunzi akabidhiwa mti wake mmoja ambao atautunza mpaka atakapohitimu elimu yake katika shule husika.
Amemalizia kwa kuwakumbusha Wanachi hasa wa jiji la Dodoma kuwa swala la usafia wa mazingira ni la kila mmoja hivyo wote wahusike katika kuhakikisha swala la usafi linapewa kipaumbele huku akiongeza kuwa endapo mtu atakiuka sheria ya usafi wa mazingira katika eneo lake basi hawatasita kuchukua hatua kali.
TAZAMA VIDEO HAPO CHINI AKIWA ANAELEZEA ZAIDI KUHUSU SWALA LA USAFI MKURUGENZI WA JIJI LA DODOMA JOSEPH MAFURU
No comments:
Post a Comment